MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI Mkurugenzi wa Kampuni ya Awino Farm, Martine (kulia) akiwa na Mtaaalamu wa Kilimo cha Papai, Ezra na Meneja wa Mashamba ya Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, Justine walipokuwa wakitoka na papai walizochuma kwenye shamba la mfano eneo la Msata, Chalinze hivi karibuni.

Na Richard Mwaikenda

Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita) umetoa ofa kwa wakulima kutandaziwa miundombinu ya umwagiliaji heka moja ya Shamba la Papai kwa sh. Mil. 2 Tu.

Ofa hiyo imetolewa Leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange kwa wanachama wa mtandao huo wenye nia ya kuwekeza kwenye zao hilo.

Ngamange amesema kuwa katika Mpango huo wataitumia Kampuni ya Awino Farm yenye  wataalamu waliobobea kwenye Kilimo cha zao hilo.

Alisema kuwa wawekezaji wa zao hilo watanufaika kwa kupata Mbegu bora za Papai aina ya Malkia inayopendwa na kuuzika kirahisi ndani na Nje ya nchi.

Pia watanufaika kwa kupangiwa bajeti ya kulima heka moja yenye gharama nafuu, ikiwemo Mbegu, mbolea na bembejeo zingine.

Heka moja unaweza kupanda miche 1200 ambapo mmoja unazaa Kati ya Papai 100 hadi 130 kila moja likiwa na uzito wa wastani wa kilo mbili.

Kutokana na kuwatumia wataalamu hao ambao pia ni mwanachama wa Mkikita, Mwekezaji ataanza kuonja matunda kwa kuanza kuvuna Papai baada ya miezi 6 Tu tangu yapandwe.

 Ngamange, amesema kuwa mkulima kwa heka moja  anaweza kupata hadi sh. Mil.80 kwa mavuno ya kwanza endapo ataamua kuuza kila Papai sh. 800 kutokana na kila mche kuzaa Papai 100. Heka moja ya Papai inakuwa na miche Kati ya 1000 hadi 1200.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

NAMAINGO YAZINDUA HEKA 7000 ZA MASHAMBA MJI KIJIJI CHA MSOLWA, MKURANGA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

HABARI MPASUKOOO:GARI LAGONGA WATOTO KUIKWEPA BODABODA GONGO LA MBOTO

HARAMBEE YA UJENZI HOSPITALI YA MUHEZA YAVUKA MALENGO, ZAPATIKA BIL. 1.6

WAZIRI SHONZA AMJIBU DIAMOND

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

HABARI MPASUKOOO!!! MCHAWI ADONDOKA AKIWA UCHI KIVULE,DAR