DKT NCHIMBI ATOA SH. MIL 10 KUWAFARIJI WAATHIRIKA WA MAPOROMOKO MLIMA KAWETERE MBEYA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Emmanuel Nchimbi ametoa kwa niaba CCM sh. mil. 10 kwa walioathirika na maporomoko ya ardhi ya Mlima Kawetere katika Kata ya Itezi jijini Mbeya.


Dkt. Nchimbi ambaye aliambatana na  wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla pamoja na Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu ametoa pole hiyo alipowatembelea kwa lengo la kuwafariji waathirika 51 waliohifadhiwa katika Shule ya Msingi Tambukareli Aprili 17, 2024.

 Kiongozi huyo mtendaji mkuu wa CCM, yupo Mbeya ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya siku 10 katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.


Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha uhai wa chama, kutatua kero za wananchi, kuelezea maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani, kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.

Baada ya kumaliza katika mikoa ya Katavi, Rukwa na Songwe, ziara hiyo ya siku 10 yenye mafanikio makubwa, itaendelea leo katika Mkoa Mbeya na hatimaye katika mikoa ya Njombe na Ruvuma.

Dkt Nchimbi akikabidhi fedha hizo kwa Fariji Nickson aliyepokea kwa niaba ya waathirika wenzie.
Dkt Nchimbi akiwapa mkono wa pole waathirika wa maporomoko hayo.









 Mwathirika Fariji Nickson akitoa shukrani kwa CCM kwa kuwapatia msaada huo muhimu kwao hasa katika kipindi hiki.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI