RAS KILIMANJARO NA DEREVA WAFARIKI KWA AJALI, MKUU WA MKOA ADHIBITISHA


 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amethibitisha kifo cha Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro Tixon Nzunda kilichotokea kwa ajali ya gari, ambapo amesema "ajali hiyo imetokea muda wa saa nane kuelekea saa tisa mchana leo, Juni 18, 2024".

"Ni kweli wakati anatoka KIA amepata ajali mbaya sana, ndio na mimi nakwenda eneo la ajali,"-amesema RC Babu

Aidha pia Dereva wa Katibu Tawala huyo Alphonce Edson amefariki Dunia katika ajali hiyo.

Babu amebainisha kuwa muda mfupi kabla ya ajali hiyo, Marehemu Nzunda alikuwa na kikao na wadau wa maendeleo kutoka nchini Namibia kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.




Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

DEMU KAMA ANAFANYA KAZI HIZI KUWA MAKINI NAE.

KAMATI YA UWT KUTOA MSAADA WA KISHERIA NCHINI

KIKOSI CHA CBE KIMEWASILI ZENJI KUVAANA NA YANGA

YANGA YAWASILI SALAMA ETHIOPIA