NJIA SITA ZA KUMNASA DEMU MKALI


 KUNA watu wamezaliwa wakiwa na hofu kubwa ya kuwaogopa mademu wazuri. Kuna mwingine akimuona demu mzuri mtaani, anajisemea kabisa kwamba; yule si taipu yangu, eti kisa kapendeza, msafi na anaonekana matawi fulani ya juu.


1. TAFUTA JINA LAKE KWANZA

Unapomtaka demu mkali mtaani kwako, kitu cha kwanza tafuta jina lake. Hii itakusaidia kumshangaza. Wanawake wapo hivi, huwa hawapendi sana kujulikana, inapotokea msichana huyo ukaonana naye na kumuita jina lake, kwanza atasimama, atakuuliza umenijuaje? Nani kakwambia jina langu? Usiogope, kwanza tabasamu, hilo litamfanya kuona kwamba wewe ni mtu mzuri, jibu utakalompa, hakikisha linakuwa lile la kukutafuta baadaye.


2. USIMLETEE SANA SHOBO

Akikupa namba, usijifanye kuwa na haraka ya kumtafuta. Unachotakiwa kufanya ni kucheza na akili yake kwanza. Najua atakuwa na hamu ya kupata simu yako, kwa siku hiyo mkaushie mpaka kesho yake ndipo umtafute. Kuwa makini, usimpigie, wewe mtumie meseji.


3. MPIGIE SASA, ANZA KUMSIFIA

Wanawake wanapenda sifa, wanapenda kusifiwa. Kitu cha kwanza mwambie kwamba kuna siku uliwasikia washikaji wakimzungumzia, kwamba demu fulani mkali, anajua kuvaa, ananukia vizuri, ukataka kumjua ndipo wakasema kwamba ni yeye.


4. KUWA MAKINI KWENYE MTOKO WAKO

Demu yeyote anapenda mwanaume mchangamfu, jinsi utakavyomuonyeshea uchangamfu kwenye simu iwe hivyohivyo hata ukionana naye na kutembea naye. Usimuonyeshee akahisi yule wa kwenye simu ni tofauti na huyu.


5. NENDENI MNAPOKWENDA

Usitake kutumia sana pesa, usitake kuingia gharama kubwa kwani mademu wana kawaida ya kumsoma mwanaume siku ya kwanza tu.


6. MALIZIA KWA KUMWAMBIA HIVI…

Mkiachana na kurudi nyumbani, mpigie simu, mwambie unamisi uwepo wake, ungetamani uwe naye tena, unaimisi harufu yake, mwambie ulikuwa karibu na ua kwa hivyo ile harufu yake imekupata hata wewe. Mchekeshe kidogo, mwambie unamisi tabasamu lake, mwendo wake wa twiga, mwambie unamisi uzuri wake, yaani huo ndiyo muda wa kumsifia mpaka ajione duniani hakuna mwanamke kama yeye.


Ukifanya hayo, jua kwamba huyo mwanamke lazima akukubali kwani atahisi yupo na mtu sahihi. Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine bomba zaidi mtag rafiki yako unayempenda ajifunze hapa!

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

KAMATI YA UWT KUTOA MSAADA WA KISHERIA NCHINI

KIKOSI CHA CBE KIMEWASILI ZENJI KUVAANA NA YANGA

YANGA YAWASILI SALAMA ETHIOPIA

DEMU KAMA ANAFANYA KAZI HIZI KUWA MAKINI NAE.