Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi amemuhakikishia mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa atamsaidia kwa uwezo wake wote na kwa uaminifu ili atekeleze Ilani ya CCM kama alivyokusudia.
Dkt. Nchimbi ameyazungumza hayo leo Jumapili Septemba 21, 2025 mbele ya Dkt. Samia Pamoja na Wananchi wakati wa mkutano wa hadhara wa Kampeni za chama hicho,uliofanyika wilayani Nyasa, Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Comments