KISHINDO CHA BALOZI DK.NCHIMBI AKIWANADI WAGOMBEA UBUNGE CCM DAR .

MGOMBEA Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi leo Septemba 28,2025 amefanya mkutano mkubwa wa kampeni katika  Uwanja wa Mwenbe Yanga jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano huo,Dkt.Nchimbi pia alipata nafasi ya kuwanadi baadhi ya wagombea Ubunge wa mkoa huo akiwemo Mbunge wa jimbo la Temeke,Ndugu Mariam Kisangi pamoja na Madiwani.

Dkt.Nchimbi ni Mgombea mwenza wa Dkt Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 wakipeperusha bendera ya CCM.

Mpaka sasa   mkoa wa Dar es Salaam unakuwa wa 15 kufikiwa na Dkt Nchimbi katika kusaka kura za ushindi  wa Kishindo za Mgombea Urais wa chama hicho Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge pamoja na Madiwani. @ccmtanzania @samia_suluhu_hassan @nchimbie #KazinaUtuTunasongaMbele











 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MBINU ZITAKAZOKUFANYA USIISHIWE PESA

DKT. MIGIRO AKIWASHA KAMPENI ZA DKT. SAMIA MAKAMBAKO

LEO NI LEO KAMPENI ZA DKT. SAMIA SONGWE

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NENO KUNTU LA UMMY MWALIMU ALILOLITOA BAADA YA KUTEMWA KUGOMBEA UBUNGE

CHONGOLO AMKUMBUKA DKT. ASHA-ROSE MIGIRO-