KIGOGO CHADEMA ATIMKIA CCM BAADA YA KUVUTIWA NA UONGOZI BORA WA DKT. SAMIA

‎Na Richard Mwaikenda, Ilala

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kanda ya Kusini, Aden Mayalla amekikimbia Chama hicho na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada kuvutiwa na uongozi bora wa Mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

‎Akizungumza baada ya kupewa fursa ya kutoa salamu katika mkutano wa kampeni za Dkt. Samia, Kinyerezi Ilala, Dar es salaam leo Oktoba 22, 2025, Mayalla ametaja sababu nyingine ya kutimkia CCM kuwa.ni kitendo cha Dkt. Samia kwamba akichaguliwa Oktoba 29, atahakikisha mchakato mpya wa katiba utaanza.

‎Mayalla ambaye pia alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, ametaja sababu  zilimfanya akihame kuwa ni uwepo wa unyanyasaji na ubaguzi uliokithili kati ya kambi za walioshinda na walioshindwa katika chaguzi zao. chama hicho kutokuwa na Future, ajenda ya kutoshiriki uchaguzi mkuu na kutokukubaliana na kitendo Cha kuandamana kupinga.uchaguzi mkuu Oktoba 29.

‎Ametoa wito kwa Watanzania kuachana upuuzi huo wa kuandamana bali washiriki ipasavyo katika Uchaguzi Mkuu na kuhakikisha wanampigia kura za kishindo Mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. Samia kwa vile ana uwezo mkubwa, ameupiga mwingi katika kuliletea Taifa Maendeleo ya dhati.


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

KIGOGO WA CHADEMA AHAMIA CCM

RAIS SAMIA SIO RAIS JOYCE BANDA WA MALAWI, TANZANIA SIO KENYA

RAIS SAMIA AMZAWADIA NYUMBA SIMBU