๐๐▫️Najua ushafundishwa namna ya kukata kiuno, najua ushafundishwa namna ya kumpikia mwanaume,
๐๐▫️Najua ushafundishwa namna ya kumheshimu na kumnyenyekea,
๐๐▫️Lakini kama usipojua namna ambavyo akili ya mwanaume hufanya kazi basi miezi mitatu tu ya ndoa utaanza kuiona ndoa chungu.
๐๐▫️Yaani pamoja na viuno vyako, pamoja na kuvumilia kwako, pamoja na kupika kwako vizuri lakini bado utaona mumeo hana shukurani, hakujali, anakudharau kwakua tu hujui namna ya akili yake inafanya kazi.
๐๐▫️Binafsi naamini mwanamke ana nguvu kubwa sana katika ndoa kwa ujumla, lakini ni wanawake wachache sana ambao hutumia nguvu hiyo.
๐๐▫️Labda nikuambie kitu kimoja, wakati wewe umefundishwa yote hayo, mwanaume kafundishwa kitu kimoja kwamba angalia mkeo asijekukukalia, asikutawale.
๐๐▫️Yaani kwa mwanaume hata kama ukiwa unakata kiunoa kama shetani lakini akihisi tu umemkalia unamuendesha basi labda umloge lakini kwa akili ya kawaida utaiona ndoa chungu.
๐๐▫️ Mwanaume hawi mwanaume kama anahisi anaendeshwa na mwanamke hata kama haendeshwi.
๐๐▫️Labda unaweza kusema mbona mimi simuendeshi, mbona mimi namtii nina nidhamu nafanya kile anachokitaka.
๐๐▫️Sasa hembu nikupe mifano tu ya mambo ya kawaida, mumeo kachelewa unamuuliza ulikua wapi?
๐๐▫️Mumeo katoka nje kupokea simu unamuuliza ulikua unaongea na nani, mumeo umemkuta kasimama na mtu ushamuambia yule ni nani na ulikua unafanya nini?
๐๐▫️Inawezekana umeuliza kwa taratibu kabisa tena kistaarabu lakini kwa mwanaume kama unaonyesha kuwa unampangia basi anaona umemkalia.
๐๐▫️Sasa ufanye nini?
๐๐▫️Nikitu rahisi tu muache ajihisi kakutawala yeye lakini kumbe unampangia kila kitu wewe.
๐๐▫️Tuchukue mfano wa kawaida, unaona mume wako anachelewa kila siku kurudi nyumbani, ndoa yenu changa na umechoka hiyo hali.
๐๐▫️Ushauliza sana na majibu yake hayaeleweki, nikuambie hata ukiita na ndugu na viongozi wa dini hataacha kuchelewa.
๐๐▫️ Lakini hembu panga muda wa chakula cha usiku, halafu jifanye huwezi kula chakula peke yako.
๐๐▫️Sasa hapa akichelwa, hutalalamika kwanini anachelewa utakua ukilalamika kwanini anapedna kula vyakula vya baridi.
๐๐▫️ Yaani utakua unasema unajali madhara, chakula kinatakiwa kiwe cha moto bhana.
๐๐▫️Kwa maana kua unalalamikia afya yake, hapa hutakua unalalamika kama mwanamke mwenye wivu ambaye anapenda kumcontrol mume wake bali mwanamke mwenye upendo ambaye hujali afya ya mumewe.
๐๐▫️Hapo akili ya mumeo itaanza kuwaza ananijali na si ananiconrtrol, kwamba wakati anaongea na wanaume wenzake hatasema huyu mwanamke ukichelewa anakasirika bali mke wangu hapendi nile vyakula vya baridi.
๐๐▫️Kumbe kichwnai wala hujali kama anakula viporo wala nini unajali kama anawahi nyumbani.
๐๐▫️Lakini kuna mambo mengine pia, unaweza kumfanya kuwa rafiki yako, kutengeneza hobi ya pamoja na vitu vya kufanya pamoja ambavyo vinamlazimisha kuwahi.
๐๐▫️Ukijua akili ya mwnaaume inavyofanya kazi mwanaume hatakusumbua.
๐๐▫️ Lakini ukiishia kukata viuno halafu kila siku kelele utashangaa, ndoa ya miezi sita ishaanza kunuka na hakuna mtu wa kukusaidia.
*๐๐▫️KUWA MBUNIFU WA KIMAWAZO NA KIMATENDO KWA MUMEO, WACHA KUJILALAMIKIA OVYO, UTACHOKWAAA!!๐*

Comments