Wengi tunamjua Fistoni Maleye anayecheza Pyramid na aliyecheza Young Africans lakini wengi hatumjui wakati wa udogo wake pamoja na makuzi ya soka.
Kutoka kuwa Hasla mpaka kuwa mfalme wa soka la Afrika kwa Mayele ni hatua kubwa sana.
Historia tamu ya Mayele mpaka hivi sasa nikufanikiwa kuchukua Kombe la ligi ya Mabingwa Barani Afrika akiwa na Klabu ya Pyramid.
Mayele alipitia changamoto nyingi za maisha wakati anajitafuta, alikwenda nchini EUA katika klabu ya Al Jazeer na alishindwa kujiunga na timu ya wakubwa baadaye alipelekwa timu ya vijana kurejesha kiwango chake ilishindikana na kurejea
njini Congo (๐จ๐ฉ).
Wakati wengine wakipata mkataba rasmi wakuvitumikia vilabu mbalimbali wakiwa na umri mdogo mpaka miaka 18, Mayele alipata mkataba wake wa kwanza akiwana na miaka (25).
Stori yake nzuri ya maisha ya soka yalianza pale AS Vita, ndio nyota yake ilianza kung'aa pale ndipo baadaye 2021 Young Africans wakamtambulisha kama mshambuliaji wao rasmi.
Utambulisho wake haukuwa wa kushtua lakini yeye ndio amewashtua watu waliokuwa wanamkatia tamaa na sasa ni Role Model wa kila mchezaji Afrika.
Alivyokuja Yanga ameifungia zaidi ya magoli 50 na kutwaa tuzo ya Mchezaji bora wa ligi kuu ya NBC na tuzo ya mfungaji bora.
Alikuwa pia mfungaji bora wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika akiwa na Yanga.
Misimu miwili ndani ya Pyramid kabeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika na Tuzo ya mchezaji bora Afrika.
Mafanikio ya Mayele yote ameyapata ndani ya miaka sita (6) tuu

Comments