Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwa Serikali imeanza kuchukua hatua za kuunda Tume ya Maridhiano ya Kitaifa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha umoja, amani na mshikamano nchini.
Rais Samia amesema tume hiyo italenga kushughulikia tofauti za kijamii na kisiasa kwa njia ya mazungumzo.
Akihutubia taifa, Rais Samia amesema Serikali itashirikiana na wadau mbalimbali kukubaliana kuhusu muundo wa tume, aina ya wajumbe, majukumu yao na muda wa utekelezaji wa kazi hiyo. Amesisitiza kuwa tofauti za kiitikadi zisiruhusiwe kuligawa taifa.
Rais Samia amewashukuru wananchi pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kudumisha amani na utulivu mwaka 2025, licha ya changamoto zilizojitokeza. Amesema Tanzania imeendelea kuthibitisha kuwa ni taifa imara na lenye uwezo wa kushughulikia changamoto zake.
Aliongeza kuwa mwaka 2026 Serikali itaendelea kuimarisha diplomasia ya uchumi na ushirikiano wa kimataifa kwa manufaa ya maendeleo ya taifa.

Comments