HAMASA YA UTALII WA NDANI DODOMA HAKUNA KULALA


NA MWANDISHI WETU

OFISI kiunganishi wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro iliyopo Dodoma imeendelea kufikia makundi mbalimbali ya taasisi za umma na binafsi, shule pamoja na wadau mbalimbali kutoa elimu ya uhifadhi na utalii sambamba na kutangaza bidhaa za utalii zilizoko eneo la hifadhi ya Ngorongoro.


Kwa mujibu wa Mkuu wa Ofisi Kiunganishi ya Ngorongoro iliyoko Dodoma Afisa Uhifadhi Mkuu Lowaeli Damalu kazi ya kutoa elimu na kutangaza utalii wa ndani kwa mikoa ya kanda ya kati inayojumuisha Singida na Dodoma ni endelevu kuhakikisha kuwa elimu ya vivutio vya utalii na shughuli za uhifadhi katika eneo la Ngorongoro zinatangazwa hasa kwa wanafunzi na taasisi za elimu ambao ni mabalozi wazuri wa kurithisha vizazi ambavyo ndio jeshi la uhifadhi wa aliasili kwa siku zijazo


Kwa upande wake Afisa Elimu Maalum wa Jiji la Dodoma, Mwalimu Issa Kambi, ameeleza kuwa jitihada za Ngorongoro kuhamasisha utalii wa ndani na kuhimiza uhifadhi wa mazingira ni ishara ya kujali wanafunzi ambao ndio nguzo ya taifa la kesho.  Wanafunzi wa shule za Dodoma ikiwemo shukl ya msingi Dodoma Viziwi wametoa shukrani kwa Mamlaka ya Uhifadhi Ngorongoro kwa kuwatembelea na kuahidi kuwa mabalozi wa utunzaji wa mazingira na kutangaza vivutio vya utalii majumbani mwao.


Eneo la hifadhi ya Ngorongoro lina utitiri wa vivutio vya utalii vinavyojumuisha utalii wa kuona Wanyama, utalii wa picha, utalii wa malikale, miamba, jiolojia, misitu, ndege, mazingira. Wageni wanaofika Ngorongoro wanapata fursa ya kutembelea na kuona eneo la Olduvai na Laetoli ambayo yana gunduzi za masalia mbalimbali ya historia ya binadamu na mambo kale.





Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Wasifu wa Kizza Besigye

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

KATI YA WATOTO 7 WA HAYATI MAGUFULI ANAYEJULIKANA ZAIDI NI JESCA

AINA 10 ZA WANAWAKE AMBAO BIBLIA INAKUONYA UWAEPUKE

KIKOSI KILICHOITWA TAIFA STARS HIKI HAPA

UBORA UNAONEKANA: BENKI YA NMB YANG'ARA TUZO ZA EUROMONEY 2026

MAJANI YA MAPERA NA MATUMIZI YAKE YA KITIBA

MCHIMBAJI MDOGO WA DHAHABU AFANYA MAKUBWA KWENYE HUDUMA ZA AFYA