RAIS SAMIA AMBADILISHA KAZI BOSI WA TCRA, MATINYI APELEKWA ALGERIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wa taasisi za kiserikali, mshauri wa Rais na kumpangia kituo cha kazi Balozi mmoja.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 24 Aprili, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Rais Samia amemteua Mhandisi Peter Phillip Mwasalyanda kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Mwasalyanda alikuwa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), na anachukua nafasi ya Dkt. Jabiri Kuwe Bakari ambaye amemaliza muda wake.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Nchi amemteua Dkt. Jabiri Kuwe Bakari kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA). Dkt. Bakari anachukua nafasi ya Bw. Salim Ramadhani Msangi ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Aidha, Rais Samia amemteua Mhe. Angela Charles Kizigha kuwa Mshauri wa Rais, Masuala ya Jamii. Vilevile, Rais amempangia Balozi Mobhare Holmes Matinyi kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

AINA 10 ZA WANAWAKE AMBAO BIBLIA INAKUONYA UWAEPUKE

MAJANI YA MAPERA NA MATUMIZI YAKE YA KITIBA

RAIS ALİYEISHI KAMA MUNGU WAKATI WATU WAKE WAKIFA NJAA

ZIJUE TIBA ZA MMEA WA MSHONA NGUO.

CHATANDA ASHIRIKI KIKAO CHA BODI HOSPITALI YA RUFAA DODOMA