FCC IMESHUGHULIKIA MALALAMIKO 63 YA WALAJI WADOGO NCHINI


Wizara Viwanda na Biashara kupitia FCC imeendelea na juhudi za kupambana na bidhaa bandia na  kumlinda mlaji dhidi ya mienendo potofu, hadaifu na kandamizi katika soko la bidhaa na huduma. 

Hayo yameelezwa na Waziri wa wizara hiyo, Judith Kapinga alipokuwa akiwasilisha hotuba ya makadirio ya Bajeti ya wizara kwa mwaka wa fedha wa 2026/2027 bungeni Dodoma Mei 22, 2026.

Amesema hadi kufikia Aprili, 2026, Wizara kupitia FCC imeshughulikia malalamiko 63 ya walaji wadogo ambapo malalamiko 45 yalipatiwa ufumbuzi na malalamiko 18 yaliyobaki  yapo katika hatua mbalimbali za utatuzi;

Aidha, Waziri Kapinga amesema kuwa FCC imesajili na kuthibitisha mikataba 27 inayoandaliwa na upande mmoja (SFCC) kwa lengo la kuondoa masharti kandamizi kwa walaji; 

"FCC imefanya kaguzi za kushtukiza 31 ambapo bidhaa zenye thamani ya shilingi bilioni 4.74 zilikamatwa kwa kuvunja Sheria ya Alama za Bidhaa ya 1963 (kama ilivyorekebishwa). "

Ametaja bidhaa zilizokamatwa kuwa ni; vipuri vya magari, vilainishi vya magari, pombe kali, vyandarua, dawa za viatu na betri.

 "Vilevile, imeendelea na ukaguzi wa kila siku wa mizigo (cargoes) ya bidhaa zinazoingizwa nchini kupitia Bandari na Bandari kavu zote (ICDs) na vituo vya pamoja vya mipakani."

 Kati ya mizigo ya bidhaa 4,791 iliyokaguliwa, mizigo ya bidhaa 418 ilikamatwa kwa kukiuka Sheria ya Alama za Bidhaa Sura ya 85. 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

TANZIA;.KWA KHERI DADA YETU MPENDWA EDITHA, TASNIA IMEPATA PIGO

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

NATAKA TANZANIA, KENYE NA UGANDA IWE NCHI MOJA, ILI BAHARI YA HINDI IWE YETU SOTE - MUEVENI

RAIS SAMIA AWASILI IRINGA KWENDA MEI MOSI NJOMBE