MKOA WA MBEYA UMEBARIKIWA

Mbeya ni Mkoa uliobarikiwa sana kwa kuwa na ardhi nzuri pamoja na hali ya hewa inayofanya vizuri katika  kilimo na ufugaji.
Kila Wilaya ndani ya mkoa wa Mbeya ina uwezo wa kuzalisha chakula cha kutosha kwa matumizi ya watu wake.
Wilaya ya Rungwe yenye halmashauri mbili (Rungwe na Busokelo) ina uzalishaji zaidi katika mazao ya Ndizi, Viazi, Mahindi, parachichi, Maharage, tangawizi, Mboga mboga na matunda" huku ikizalisha mamilioni ya lita za maziwa ya ng'ombe kwa mwaka.
Kwa takwimu za mwaka 2022 halmashauri ya Busokelo pekee ilitajwa kuzalisha lita milioni 42 za maziwa ya ng'ombe kwa mwaka.

Wilaya ya Mbeya yenye halmashauri mbili (Mbeya jiji, na Mbeya) ni kinara wa uzalishaji wa mazao kama viazi, maziwa, kahawa, karoti, matunda, Mahindi na maharage.
Soko la Karoti na matunda (Igawilo Darajani) ni tegemeo kwa wafanyabiashara wengi wa ndani na nje ya nchi.

Si hivyo tu, mchele kutoka Wilaya Kyela unafanya vizuri katika masoko mbalimbali ya chakula ndani na nje ya nchi hivyo kuendelea kuaminika kwa ubora wake. kilimo cha Mpunga kinashika kasi wilayani Kyela kama ilivyo kwa mazao mengine kama Kokoa na michikichi "Mawese".

Wilaya ya Mbarali ni kinara wa uzalishaji wa Mpunga mkononi Mbeya ikiwa na mashamba makubwa ya wawekezaji na wakulima wadogo wadogo, Mchele wake huuzwa nchini na mataifa mengine ukiwa na ubora wa kuaminika.

Mbali na shughuli za uchimbaji madini ya zahabu, Wilaya ya Chunya haijajitenga na kilimo kwani ina uzalishaji mkubwa wa mazao ya Mahindi, Maharage tumbaku, na mazao mengine kibao yanayotumika kwa chakula na biashara.

Mbeya imekuwa kimbilio la wasaka maisha, wanaokimbia njaa na ugumu wa maisha kutoka mikoa mbalimbali yenye upungufu wa chakula na ugumu wa maisha.

Watumishi wa umma ambao si wenyeji waliopangiwa kufanya kazi Wilaya za mkoa Mbeya wengi hukataa kuhamishiwa mikoa mingine kwa kwa sababu ya maisha mazuri wanayoyapata ndani ya vijiji na miji ya Mbeya.


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

TANZIA;.KWA KHERI DADA YETU MPENDWA EDITHA, TASNIA IMEPATA PIGO

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

NATAKA TANZANIA, KENYE NA UGANDA IWE NCHI MOJA, ILI BAHARI YA HINDI IWE YETU SOTE - MUEVENI

RAIS SAMIA AWASILI IRINGA KWENDA MEI MOSI NJOMBE