Na Victor Masangu,Pwani
Mkuu wa mkoa wa Pwani Alhaj Abubakar kunenge amewataka watendaji wa Kata kuhakikisha wachapa kazi kwa weledi na bidii ikiwemo kushughulikia changamoto mbali mbali zinazowakabiliwa wananchi ikiwemo kero zinazohusiana na migogoro ya ardhi na kuepukana kabisa na uuzaji wa ardhi kiholela bila ya kuzingatia taratibu zilizowekwa.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa kikao kazi na watendaji wa kata zote zipatazo 136 zilizopo katika Mkoa wa Pwani kikiwa na lengo la kujweza kujadili mambo mbali mbali ya kiutendaji pamoja na kukumbashana namna wanavyopaswa wawajibike katika suala zima la kusikiliza kero na changamoto ambazo zinawakabili wananchi ili waweze kuzitatua na kuzitafua ufumbuzi.
Kunenge amesema kwamba viongozi pamoja na watendaji wanapaswa kutoa huduma kwa wananchi hivyo ana imani kikao kazi hicho kitaweza kuleta mageuzi makubwa katika suala zima la uwajibikaji kwa wananchi pindi wanapokuwa katika maeneo yao ya kazi.
"Tumeamua kuwakutanisha watendaji wetu wote wa kutoka kata zote 136 za Mkoa wetu na dhamira yetu kubwa ni kukumbushana mambo mbali mbali ambayo wanapaswa kuyasimamia pindi wanapokuwa katika maeneo yao na kikao hiki nimeamua kuwakutanisha watendaji tu kwani wao ndio kiungo kikubwa maana ndio wapo karibu na wananchi na wanatambua changamoto zao katika maeneo husika,"amesbainisha Kunenge.
Aidha amewahasa watendaji hao kuhakikisha kwamba wanaweka misingi imara ya kufuatilia na kusimamia shughuli za utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwa pamoja na suala zima la kuongeza juhudi zaidi katika ukusanyaji wa mapato lengo ikiwa ni kuisaidia serikali ya awamu ya sita kupata mapato yake.
Katika hatua nyingine amewahimiza kuzingatia vipaumbele vya serikali na lengo kubwa likiwa ni kuwahudumia wananchi ipasavyo na kuwasikiliza changamoto zao katika sekta ya afya, elimu, maji, miundombinu ya barababara, nishati ya umeme,kilimo, pamoja na mahitaji mengine ya msingi kwa lengo la kuzifanyia kazi ikiwa sambamba na kuboresha maisha yao ya kila siku.
Nao baadhi ya watendaji ambao wamehudhulia katika kikao kazi hicho akiwemo Francis Shawa Mtendaji wa Kata ya Misugusugu wamempongeza Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa kuweza kuona umuhimu wa kuwaita pamoja na kuwapa mahalifa ya kuwakumbusha mambo muhimu yanayopswa kufanyika katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Wamesema kwamba wameweza kupata mahalifa na elimu zaidi ambayo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani na kuahidi kwenda kuyafanyika kazi yale yote ambayo wameagiza pindi watakaporejea katika maeneo yao ya kazi.
"Kwa kweli sisi kama watendaji wa kata tumefarijika sana kukutana na kikao kazi hiki amabncho kwa kweli kimetukutanisha na watendaji wengiine kutoka maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Pwani lakini kipekee nimshukuru Mkuu wetu wa Mkoa wa kuamua kutukumbusha mambo mbali mbali ambayo ni muhimu sana hasa sisi ambao tunakutana na wananchi katika ngazi za chini na tunaahidi kuyafanyia yote ambayo tumeelekezwa,"amebainisha Shawa.
Kikao kazi cha watendaji kutoka kata zote 136 za Mkoa wa Pwani kimeandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambapo pia ndiye aliyekuwa mkufunzi na kuwasilisha mada mbali mbali ambazo zimeweza kuletaa tija zaidi kwa watendaji hao kutokana na kufahamu mambo tofauti ambayo yataweza kuwasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao ya kikazi.

Comments