Ni kwamba rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Nyerere alifanya ziara ya kiserikali huko Urusi ama Soviet Union kwa mara ya kwanza ambayo pia ilikuwa ya mwisho kwa kiongozi Mkuu wa Nchi mnamo Oktoba 1969. Kwa sasa imepita miaka 56!!!
Rais Samia Suluhu Hassan sasa yupo Moscow kwenye ziara ya kiserikali kwa mwaliko wa Rais Vladimir Putin. Hii ndiyo ziara ya pili tu ya Rais wa Tanzania kwenda Urusi tangu Nyerere 1969.
Rais Samia mwenyewe amesema ni "alama muhimu, baada ya zaidi ya miongo mitano".
Kwa upande wa viongozi wa ngazi ya juu wa Urusi kuja Tanzania, hakuna ziara ya Rais wa Urusi iliyoripotiwa hadharani. Lakini mawaziri na wajumbe wamekuwa wakija mara kwa mara:
👉Sergey Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, amekutana na viongozi wa Tanzania Cairo na Moscow.
👉Sergei Kiriyenko, mjumbe maalumu wa Putin, alileta ujumbe maalum Ikulu Chamwino Dodoma Novemba 2025.
Tanzania na Urusi zimekuwa na uhusiano wa urafiki wa muda mrefu tangu Tanganyika ipate uhuru 1961. Soviet Union ilikuwa miongoni mwa nchi za kwanza kutambua na kuunga mkono Tanzania. Urafiki huo umeendelea miaka 60+ kwenye nyanja za ulinzi, elimu, nishati na biashara.
Kwa hiyo ziara ya Samia sasa ni "milestone" kubwa - inaendeleza urithi wa Nyerere 1969

Comments