PBPA YASHIRIKI WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2026 DODOMA


NA MWANDISHI WETU

WAKALA wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) umeshiriki ufunguzi rasmi wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2026 yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma. Maonesho hayo yalifunguliwa rasmi tarehe 17 Juni 2026 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwan Kikwete.



Akizungumza wakati wa ufunguzi huo,  Kikwete alisema kuwa Wiki ya Utumishi wa Umma ni jukwaa muhimu la kuwakutanisha wananchi na taasisi za Serikali kwa lengo la kuwafikishia huduma mbalimbali na kuongeza uelewa kuhusu majukumu na mafanikio ya taasisi hizo katika kuhudumia wananchi.



Maonesho hayo yanatoa fursa kwa taasisi za umma kuwasilisha huduma zao, kutoa elimu kwa wananchi na kuonesha mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa majukumu yao.


Akizungumzia ushiriki wa PBPA katika maonesho hayo, Mkaguzi wa Mafuta wa PBPA, Issa Mwitazy, alisema kuwa wakala huo unatumia maonesho hayo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Mfumo wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja na mchango wake katika kuhakikisha upatikanaji wa mafuta nchini, kuimarisha uwazi katika sekta ya mafuta na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa bidhaa za mafuta.



Alieleza kuwa wananchi wanaotembelea banda la PBPA wanapata fursa ya kujifunza kuhusu majukumu ya wakala huo pamoja na mafanikio yaliyopatikana tangu kuanza kutekelezwa kwa Mfumo wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja.


Kupitia ushiriki wake katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2026, PBPA inaendelea kuimarisha uhusiano na wadau mbalimbali pamoja na kutoa taarifa sahihi kuhusu mchango wa Mfumo wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja katika kuimarisha usalama wa nishati na kuchochea maendeleo ya uchumi wa Taifa.






Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA

UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MSALATO DODOMA KUANZA KUTUMIKA SEPTEMBA 2026

Wasifu wa Kizza Besigye

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA