RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA BENKI YA NMB TAMASHA LA UWEKEZAJI ZANZIBAR

Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametembelea banda la Benki ya NMB katika Tamasha la Uwekezaji Zanzibar 2026 lililofanyika Golden Tulip Airport Hotel, Zanzibar.

 NMB ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa tamasha hilo la kila mwaka lililowakutanisha viongozi wa serikali, wawekezaji, taasisi za fedha, watendaji wakuu na wadau wa sekta binafsi kujadili fursa za uwekezaji na ukuaji endelevu wa uchumi wa Zanzibar.

Rais Dkt. Mwinyi alipokelewa na Meneja wa Benki ya NMB, Tawi la Zanzibar, Ahmed Nassor, ambaye alimweleza kuhusu  suluhisho mbalimbali zinazopatikana kupitia NMB kwa wawekezaji, kampuni na taasisi zinazofanya kazi Zanzibar.

Akizungumza katika banda hilo, Nassor alisema ushiriki wa NMB katika tamasha hilo unaonesha utayari wa benki hiyo kuendelea kuwa mshirika wa karibu wa Serikali na sekta binafsi katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa Zanzibar.
 
“Kwa NMB, Tamasha la Uwekezaji Zanzibar ni jukwaa muhimu la kuonesha suluhisho tulizonazo kwa wawekezaji, makampuni na taasisi zinazofanya kazi Zanzibar. Tupo tayari kusaidia mahitaji yao ya kifedha kupitia huduma za kibenki, malipo, makusanyo na mifumo ya kidijitali, huku tukiendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kusukuma mafanikio makubwa zaidi ya kiuchumi kwa Zanzibar,” alisema Nassor.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

Wasifu wa Kizza Besigye

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA