RAIS SAMIA AKUTANA NA RAIS WA URUSI PUTIN

Siku ya kwanza ya ziara yangu ya kitaifa katika Shirikisho la Urusi ambapo pamoja na mambo mengine, nimepata heshima ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Rais Vladimir Putin jijini Moscow.


Kwa pamoja tumepongeza ukuaji wa biashara kati ya nchi zetu uliofikia asilimia 72 katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025. Hata hivyo, kwa kuzingatia historia kubwa ya ushirikiano na uhusiano wa kirafiki kati ya mataifa yetu, tumekubaliana kuongeza juhudi za kukuza biashara na uwekezaji ili kuleta manufaa makubwa zaidi ya kiuchumi na ustawi wa wananchi wa nchi zetu.

Aidha, kwa lengo la kufungua fursa zaidi kwa wananchi na kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi, tumejadili namna ya kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali za kimkakati, zikiwemo sayansi na teknolojia, elimu, nishati, madini, kilimo, miundombinu na utalii.








 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA