SERIKALI YAKIRI SHULE ILIYOJENGWA NA NMB INA VIWANGO

 Serikali imeipongeza NMB Bank Plc kwa kujenga shule ya sekondari ya bweni kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wilayani Bahi, mradi wa Sh5 bilioni uliokamilika kwa asilimia 100.


Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu, Atupele Mwambene, amesema shule hiyo imejengwa kwa kiwango cha juu na ina mabweni, vitanda, madawati pamoja na uwezo wa kuhudumia wanafunzi 160. Inatarajiwa kuanza kupokea wanafunzi Januari 2027 baada ya usajili.

Mkurugenzi wa Uhusiano na Wawekezaji, Uendelevu na Mawasiliano wa NMB, Innocent Yonazi, amesema mradi huo unalenga kupanua fursa za elimu kwa watoto wenye mahitaji maalumu. NMB imetoa zaidi ya Sh24 bilioni kwa miradi ya kijamii katika miaka mitano.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bahi, Albina Mtumbuka, amesema halmashauri iko tayari kuipokea na kuitunza shule hiyo, huku akiwataka wazazi kutowaficha watoto wenye mahitaji maalumu.










Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MSALATO DODOMA KUANZA KUTUMIKA SEPTEMBA 2026

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Wasifu wa Kizza Besigye

NGUVU YA UJASUSI WA TANZANIA KITOVU CHAKE NI IRINGA TANGU ENZI ZA MKWAWA