VIJANA WENYE MAHITAJI MAALUM WAITWA CHUO CHA FURAHIKA KUPATA ELIMU YA UFUNDI BURE

 


NA MWANDISHI WETU

DKT. David Msuya, Kaimu Mkuu wa Furaika Education College Tanzania, amesema chuo hicho kimejipanga kutoa elimu ya ufundi bure kwa kundi hilo kuanzia Julai mwaka huu na kwa sasa wandelea na usahili.


Ameongeza kuwa usahili huo unaoendelea ni kwa kundi hilo na wasiokuwa na mahitaji maalum kwa lengo la kuwasaidia kufikia ndoto zao za maisha kupitia elimu na ujuzi.

Akizungumza leo chuoni hapo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam, Dkt. Msuya alisema chuo hicho kimesajiliwa na NACTVET kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Maendeleo ya Jamii.

Alisema ulemavu sio kigezo cha mtu kushindwa kupata elimu, hivyo chuo hicho kimeweka mazingira rafiki kwa wanafunzi wenye changamoto mbalimbali ikiwemo wasiosikia, wenye ulemavu wa viungo na mahitaji mengine maalum.

“Tunao walimu wa saikolojia, walimu wa lugha ya alama na mazingira mazuri ya kujifunzia. Tunataka kila kijana atimize ndoto yake bila kujali changamoto alizonazo,” alisema Dkt. Msuya.

Aidha, aliwataka wazazi na mashirika mbalimbali yanayosaidia watu wenye mahitaji maalum kuwapeleka vijana hao chuoni hapo ili waweze kupata elimu na kujifunza ujuzi utakaowasaidia kujiajiri na kuendesha maisha yao.

Alisema licha ya masomo kuwa bure, wanafunzi hao wenye huitaji Maalum watachangia shilingi 20,000 na wasiokuwa na huitaji wachangia 50,000 tu kwa ajili ya mitihani ya NACTVET, huku akisisitiza kuwa mashirika yanaweza kusaidia gharama hiyo kwa vijana wasiojiweza.

Dkt. Msuya amesema chuo hicho kinatoa kozi mbalimbali za ufundi zikiwemo Ususi, Umeme, ICT, Hoteli, Udereva, Bandari na nyingine zinazomwezesha kijana kujiajiri mara baada ya kuhitimu.

“Tunataka vijana wajifunze ujuzi wa kuwasaidia kuendesha maisha yao hata kama hawajaajiriwa. Mtu akijua kushona viatu, kutengeneza umeme au kufanya kazi za hoteli anaweza kujipatia kipato kila siku,” alisema.

Pia alishukuru Serikali ya Awamu ya Sita pamoja na Wizara ya Elimu kwa kuendelea kusaidia sekta ya elimu ya ufundi nchini.

Kwa mujibu wa uongozi wa chuo hicho, usajili kwa vijana wenye mahitaji maalum unaendelea na milango iko wazi kwa Watanzania wote wanaohitaji kupata elimu ya ufundi bure.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

Wasifu wa Kizza Besigye

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA