NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya Organic Moringa Limited, imeitoa rai kwa jamii kutumia bidhaa zinazitokana na Mlonge kwa kuwa zina virutubisho vingi.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Organic Moringa, Sebastian Msapalla wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni jijini Dodoma
"Jamaii imeendelea kuzalisha bidhaa mbalimbali za asili kwa kutumia mimea yenye virutubisho, ikiwemo mlonge, uwi, rosela, mbegu za chia, mchele wa kahawia pamoja na asali inayozalishwa katika mazingira yenye miti ya mlonge," amesema.
Amesema kampuni hiyo inalenga kuwapatia wananchi bidhaa zinazotokana na maliasili na zinazoweza kutumika kama sehemu ya lishe yenye virutubisho.
Miongoni mwa bidhaa zinazotolewa na kampuni hiyo ni unga wa majani ya mlonge, ambao hutengenezwa kwa kuzingatia taratibu za usindikaji ili kuhifadhi virutubisho vinavyopatikana kwenye majani ya mlonge.
Msapalla amesema, bidhaa hiyo imeandaliwa kwa matumizi ya binadamu na inaweza kutumika kuongeza virutubisho katika lishe.
Aidha, Organic Moringa imekuja na bidhaa nyingine inayojulikana kama Moringa Root Powder, ambayo ni unga unaotokana na mzizi wa mlonge. Kampuni inaeleza kuwa bidhaa hiyo hutumika katika tiba asili, huku ikisisitiza umuhimu wa matumizi sahihi na kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya.

Comments