TANZANIA, RWANDA ZAKUBALIANA KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA MAFUTA


WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Jamhuri ya Rwanda, Antoine Kajangwe, yaliyolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda katika maendeleo ya sekta ya nishati, hususan katika sekta ndogo ya Mafuta.


Mawaziri hao wamekutana leo, tarehe 17 Agosti 2026, katika Ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, ambapo wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda, hususan katika sekta ya mafuta.


Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dkt. James Mataragio, Kamishna Mkuu (High Commissioner) wa Jamhuri ya Rwanda nchini Tanzania, Jenerali Patrick Nyamvumba pamoja na Kamishna wa Mafuta na Gesi wa Wizara ya Nishati, Goodluck Shirima.





Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Soma Taarifa ya UTEUZI:Rais Jakaya Kikwete amemteua Dkt. Ben E. Moshi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya PUMA Energy (zamani ilijulikana kama BP Ltd)

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

OWM–TAMISEMI YASHINDA TUZO YA MABADILIKO YA KIDIJITALI KATIKA TEHAMA AWARDS 2026

KOCHA WA MC ALGERS AIHOFIA YANGA

VIONGOZI NA WATENDAJI WA MATAWI UVCCM PANGANI WANOLEWA

NMB YAWAUNGANISHA WANANCHI NA HUDUMA, FURSA ZANZIBAR

HIZI HAPA TAKWIMU ZA PETER SHALULILE MCHEZAJI MPYA WA YANGA SC 🔰 🔥