TANZANIA YAICHAPA UGANDA 6-0 FEASSA 2026


NA OWM-TAMISEMI, MOROGORO


TIMU ya mwenyeji Tanzania imeendeleza ubabe katika mashindano ya Michezo ya Wanafunzi wa shule za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (FEASSA )baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Uganda katika mchezo wa soka la wasichana uliochezwa leo, Agosti 17, 2026, kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Morogoro.


Tanzania ilionyesha kiwango bora tangu dakika za mwanzo, ikitawala mchezo kwa umiliki wa mpira, mashambulizi ya kasi na matumizi mazuri ya nafasi, hali iliyoiweka Uganda katika presha kubwa.


Kwa mujibu wa taarifa za mchezo, mabao ya Tanzania yalifungwa na  Olesia Nestor, Neema Fikri, Safi Amos, Olesia Nestor, Naomi Ado na Happiness Ibrahim.


Ushindi huo wa mabao 6-0 umeongeza hamasa kwa kikosi cha Tanzania kinachowakilisha nchi mwenyeji katika mashindano hayo ya wanafunzi kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Michezo ya FEASSA yanaendelea kufanyika mkoani Morogoro, yakishirikisha timu kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi katika michezo mbalimbali.




Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

Soma Taarifa ya UTEUZI:Rais Jakaya Kikwete amemteua Dkt. Ben E. Moshi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya PUMA Energy (zamani ilijulikana kama BP Ltd)

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

OWM–TAMISEMI YASHINDA TUZO YA MABADILIKO YA KIDIJITALI KATIKA TEHAMA AWARDS 2026

KOCHA WA MC ALGERS AIHOFIA YANGA

VIONGOZI NA WATENDAJI WA MATAWI UVCCM PANGANI WANOLEWA

NMB YAWAUNGANISHA WANANCHI NA HUDUMA, FURSA ZANZIBAR

HIZI HAPA TAKWIMU ZA PETER SHALULILE MCHEZAJI MPYA WA YANGA SC 🔰 🔥