PROF. MWANDOSYA ALIPOTINGA TBL MWANZA

Meneja wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Mwanza, Richmond Raymond (mbele kushoto) akimuongoza Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya kutembelea mradi wa maji alipofanya ziara hivi karibuni kiwandani hapo, kujionea utendaji wa kiwanda hicho pamoja na mradi huo wa maji unaowahudumia bure wananchi wanaoishi karibu na kiwanda hicho. Ziara hiyo ilikuwa ni moja ya shamrashamra za maadhimisho ya Wiki ya Maji iliyofikia kilele juzi jijini Mwanza..

jijini Mwanza
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya (katikati) na wadau wengine wa maji, wakipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Uzalishaji Bia wa Kiwanda cha TBL Mwanza, Jeremia Kamambi (kushoto) walipotembelea hivi karibuni  kiwanda hicho kuona uzalishaji wa bia na juhudi mbalimbali za utunzaji na udhibiti wa matumizi ya maji ambayo ni muhimu kwa maisha ya kila siku ya Watu. Ziara hiyo ilikuwa ni moja ya shamrashamra za maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo imefikia kilele juzi

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya (kulia) akitembelea Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) cha  Mwanza, alipofanya ziara hivi karibuni katika kiwanda hicho kuona uzalishaji wa bia na juhudi mbalimbali za utunzaji na udhibiti wa matumizi ya maji ambayo ni muhimu kwa maisha ya kila siku ya Watu. Ziara hiyo ilikuwa ni moja ya shamrashamra za maadhimisho ya Wiki ya Maji iliyofikia kilele juzi jijini Mwanza.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya (kulia) Meneja wa Kiwanda cha TBL Mwanza, Richmond Raymond (kushoto) pamoja na Meneja Ubora wa Bidhaa wa kiwanda hicho, Caroline Nhonoli (katikati) alipotembelea hivi karibuni  kiwanda hicho kuona uzalishaji wa bia na juhudi mbalimbali za utunzaji na udhibiti wa matumizi ya maji ambayo ni muhimu kwa maisha ya kila siku ya Watu. Ziara hiyo ilikuwa ni moja ya shamrashamra za maadhimisho ya Wiki ya Maji iliyofikia kilele juzi jijini Mwanza.

Mwandosya akiwa ndani ya ofisi ya TBL Mwanza

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

KATIKA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA.

YANGA YAMPOTEZA MAMA FATMA KARUME MWANA YANGA KINDAKI NDAKI

𝐌𝐉𝐔𝐄 𝐊𝐀𝐂𝐇𝐄𝐑𝐎 𝐌𝐙𝐄𝐍𝐀

MAELFU WAFURIKA TIKTOK LIVE YA DHARURA YA WAZIRI GWAJIMA KUHUSU CHANGAMOTO ZA WANAUME KWENYE NDOA