Rais Jakaya Kikwete akiwa na wachezaji wa Twiga Stars, Ikulu, Dar es Salaam, baada ya kufanikiwa kuingia kwenye michuano hiyo ya All African GamesTIMU ya Taifa ya wanawake ya soka Twiga Stars leo itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Banyana Banyana ya Afrika Kusini katika michezo ya Afrika inayoendelea mjini Mpauto, Msumbiji.
Wakati wanawake hao wa soka wakiingia uwanjani wenzao wa netiboli juzi Taifa Queens waliichapa Kenya kwa jumla ya magoli 36-35 katika michezo hiyo ya Afrika.
Ushindi huo wa Taifa Queens unaweza kuwa chachu ya mafanikio ya Twiga Stars leo itapotupa karata yake ya pili katika Michezo ya Afrika inayoendelea nchini humo.
Twiga Stars walianza vibaya michuano hiyo baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1, ambapo leo wana kazi kubwa ya kuhakikisha wanashinda kabla ya kukutana na Zimbabwe katika mchezo wa mwisho.
Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Boniface Mkwasa alisema ana mategemeo makubwa na timu hiyo ambayo imeonyesha morali kubwa na kuwaomba Watanzania wazidi kuiunga mkono kwa sala.
Kwa upande wa mchezo wa netiboli, Queens walicheza kwa umakini na kufanikiwa kupata ushindi huo muhimu katika
Comments