Habari zilizotufikia punde ni Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Lewis Makame (pichani) amefariki dunia leo katika Hospitali ya AMI , Masaki jijini Dar es Salaam alilokuwa amelazwa kwa ugonjwa uliokuwa unamsumbua.
Jaji
Makame ambaye kwa kipindi kirefu aliongoza NEC, alilazwa katika
hospitali hiyo mwishoni mwa mwezi Julai. Rais Jakaya Kikwete
alimtembelea kumjulia hali Julai 28, mwaka huu.
Kwa vipindi viwili, Jaji Makame akiwa Mwenyekiti wa NEC, ndiye aliyetangaza matokeao ya uchaguzi Mkuu wa 2005 na 2010 ambapo Rais Kikwete aliibuka mshindi dhidi ya vyama pinzani.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali leo, Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Lewis Makame aliyelazwa katika hospitali ya AMI iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam Julai 28,2014.
Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi.
Habari zaidi juu ya kifo chake tutawaletea baadaye.

Comments