Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amehamisha majukumu ya sekta ya habari kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwenda Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo Profesa Paramagamba Kabudi ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo na kumteua Gerson Msigwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na kurejeshwa kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali nafasi ambayo aliwahi
ishika awali.
Awali Kabudi alikuwa Waziri wa Katiba na Sheia na Msigwa alikuwa Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Comments