Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Imeanzisha matibabu ya kuziba mapengo Vipandikizi Meno (Dental Implant), ambapo mzizi bandia hupandikizwa kwenye taya, kisha kuwekewa meno juu yake yanayogandishwa na kutumika kama sehemu ya meno yake ya kuzaliwa nayo.
Aidha, Serikali imewezesha hospitali hiyo kununua mashine ya kisasa kabisa inayowezesha uchunguzi wa magonjwa ya mifupa ya taya pamoja na CT scan ya uso na kichwa kusaidia kupanga upandikizaji wa vipandikizi vya meno ambapo tangu kununuliwa mwishoni mwa mwaka 2024 tayari wagonjwa 2,251 wamenufaika.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Huduma ya Upasuaji wa hospitali hiyo, Dkt. Rachel Mhaville alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dodoma Machi 6, 2025, kuhusu mafanikio ya MNH katika miaka minne ya ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Dkt. Mhaville ambaye kwenye mkutano huo alikuwa anazungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa MNH, Prof. Mohamed Janabi, amesema kuwa wameanzisha huduma nyingine ya kuondoa sehemu yenye ugonjwa kwenye taya kisha kuvuna sehemu ya mbavu pamoja na mfupa wa nyonga kwa kutumia vipandikizi maalum kuunda mfupa wa taya jipya la chini ili kumrejeshea mgonjwa muonekano mzuri lakini pia huweza kupandikizwa meno na kumrejeshea mgonjwa uwezo wa kula tena.
Mkurugenzi Msaidiz wa Idara ya Habari MAELEZO, Zamaradi Kawawa akitoa neno la kuhitimisha mkutano huo.
. IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
0754264203
Comments