BODI YA LIGI SASA WAOMBA HEKIMA NA BUSARA ITUMIKE DERBY YA YANGA, SIMBA


 #MICHEZO: Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mnguto, amesema tayari wamejibu barua ya Yanga na hawana mamlaka ya kuwazuia kwenda CAS lakini kama wameenda CAS kwa kipindi hiki ambapo hawajasema kuwa suala hilo limeamriwa vipi itakuwa ni kitu cha kuchekesha. 


Akisisitiza kuwa maamuzi ya mwisho ya bodi bado hayajatolewa, akiamini kuwa suluhu inaweza kupatikana kupitia vikao vya ndani. Mnguto ameeleza kuwa busara na hekima zinapaswa kutumika ili kila upande uridhike badala ya kupeleka suala hilo nje ya nchi.


''Hili jambo lazima hekima na busara itumike, Sheria, kanuni zipo kweli lakini lazima pia utumie hekima na busara, huyo asiyetaka kutumia hekima wala busara kusema kweli huyo hayupo upande wetu kutatua hilo tataizo. Nia yake ni kutengeneza tatizo jipya ambalo haitakuwa na maana yoyote, hata kuziombea timu moja kushushwa daraja unapata faida gani?'' - Steven Mnguto

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MWABUKUSI ATOA NENO SIMBA KUSUSIA DERBY DHIDI YA YANGA

RAIS TRUMP ARARUANA NA RAIS WA UKRAINE

SERIKALI YALIKUBALI OMBI LA DIAMOND

HOSPITALI YA MUHIMBILI YAANZISHA HUDUMA YA KISASA YA KUZIBA MAPENGO

MWANAMKE ALIYEVUNJA REKODI KWA KUZAA WATOTO 69

ARAJIGA AULA KOMBE LA DUNIA