Taswira ya Moshi iliyodakwa na Ankali mwaka 1993 ikionyesha mapambazuko na Mlima Kilimanjaro ukichomoza, ni kumbukumbu ya mji huu mdogo ulioko kaskazini mwa Tanzania.
Moshi hujivunia kusimama chini ya kivuli cha Kilimanjaro — mlima mrefu zaidi Afrika na wa kipekee duniani kusimama peke yake bila safu nyingine ya milima.
Ingawa jina “Moshi” mara nyingi huhusishwa na mvuke wa mlima, baadhi ya wanaisimu husema limetokana na neno la Kichagga "Moshiri", likimaanisha “eneo la kati” au “mpakani.” Makinikia ya jina hilo bado yanatafutwa.
Moshi ni mji wa kihistoria na kitovu cha maendeleo ya kaskazini mwa Tanzania tangu mwishoni mwa karne ya 19.
Ulikuwa makao ya utawala wa Kijerumani na baadaye Kiingereza, na ndipo taasisi nyingi za mwanzo za kiserikali na kidini zilipoanzia.
Mji ulianza Old Moshi na baadaye ukapanuka kuelekea Moshi mjini katika karne ya 20.
Mwaka 1899, Wachagga walivamia Arusha kuwakomboa ndugu zao waliotekwa na Wamasai — wakati huo Arusha haikuwa hata mji rasmi, bali ilitawaliwa kutoka Moshi. Hii inaonesha Moshi ulikuwa mbele katika maendeleo.
Wajerumani walipoujenga reli kutoka Tanga hadi Arusha kupitia Moshi ili kusafirisha kahawa, uchumi wa mji ulipaa sana kimaendeleo.
Baada ya vita, Waingereza waliendeleza miundombinu. Moshi ukawa kitovu cha elimu, afya na siasa, huku taasisi kama KCMC na KNCU zikichangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kijamii na harakati za uhuru.
Leo, mji wa Moshi umeendela kuwa lango la mkoa wa Kilimanjaro, mji wa utulivu unaopumulia historia.
Comments