MWABUKUSI ATOA NENO SIMBA KUSUSIA DERBY DHIDI YA YANGA


 Kufuatia kile ambacho kimetokea usiku wa jana kwa klabu ya Simba kuzuiwa kufanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, na kueleza hawatashiriki mchezo wa Dabi ya dhidi ya Yanga SC.


Kupitia mtandao wa X zamani (Twitter) Rais wa Chama cha WanaSheria Tanganyika (TLS) Wakili Boniface Mwabukusi ametoa neno.


"Hata kama Simba imezuiwa kucheza ilitakiwa ieleze imechukua hatua gani za kiuongozi kuwasiliana na wahusika baada ya kupuuzwa kwa maelekezo ya Kamishna wa Mchezo.


"Huwezi toa tamko kwa umma halafu unaacha maelezo ya msingi na kuishia kusema haki imehifadhiwa ? Ni kukosa umakini je ninyi kama club mumechukua hatua zipi za kusisitiza haki zenu katika kuitaarifu Bodi ya Ligi? au TFF?"

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

RAIS TRUMP ARARUANA NA RAIS WA UKRAINE

SERIKALI YALIKUBALI OMBI LA DIAMOND

HOSPITALI YA MUHIMBILI YAANZISHA HUDUMA YA KISASA YA KUZIBA MAPENGO

ARAJIGA AULA KOMBE LA DUNIA

MAMBO 8 MWANAMKE HUFANYA KWA MWANAUME ANAYEMPENDA