Bodi ya ligi kuu nchini Tanzania (TPLB) chini ya mwenyekiti wake Steven Mguto imeiomba klabu ya Young Africans Sports Club kusitisha harakati za kufungua kesi katika mahakama ya masuala ya soka duniani CAS kuhusu kuishitumu Bodi hiyo kwa kushindwa kusimamia vyema Sheria na kanuni za Ligi,
Bodi ya ligi inaomba klabu hiyo irudi mezani wakae kwa pamoja wamalize mzozo baina Yao Kwa busara na hekima,
Bodi ya ligi imekiri Kuna Makosa yalitokea katika kuahirisha Mchezo kinyume na taratibu lakini wanaomba yafanyike majadiliano ya kutafuta Suluhu kwa hekima na busara badala ya kanuni na Sheria,
Mpaka kufikia Sasa klabu ya Young Africans Sports Club bado haijatoa ripoti maalumu kuwa kama wapo tayari kufanya majadiliano na Bodi ya ligi.
Comments