BREAKING NEWS | MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO AFARIKI DUNIA
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Gissima Nyamohanga amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika ajali ya gari katika Wilaya ya Bunda, mkoani Mara. Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mara, Nickison Babu amethibitisha kutokea kwa ajali na kifo cha Nyamohanga na kwamba mwili wake mpaka sasa upo hospital ya DDH wilayani humo. Amesema kwasasa wanasubiri kauli ya familia ili kujua ni wapi msiba utawekwa kutokana na kuwa na makazi ya marehemu ni jijini Dar es Salaam huku kwao ikiwa ni mkoani Mara. Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba kwa sasa yupo eneo la tukio na atatoa taarifa zaidi baadaye. Chanzo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni dereva gari dogo aina Land Cruiser alijaribu kumkwepa muendesha baiskeli na kwenda kugongana na lori ambapo katika ajali hiyo, dereva wa gari la mkurugenzi nae amefariki dunia. ✍ Augustine Mgendi #AzamTVupdates
Comments