MANARA AMEANDIKA HIVI......
1- Ijumaa,Dua za familia na Mashekh zitakazofanyika Zanzibar,Kigoma na Dar
2-Jumamos,Big Party kwa Rafiki wa Bwana harusi,Ukumbi Diamond Jubilee VIP Dar
3-Jumapili kitchen Party Hotel Verde,Zanzibar
4-Jumatatu na Jumanne,Ngoma za kiasili toka Unguja na Kigoma,Shughuli hii ni Zanzibar na Dar
5-Jumatano,Hina na Sharah Zanzibar
6-Alhamis Ndoa kwenye Msikiti mdogo tena alfajiri, kukwepa Vijicho na hasadi.
Mchana karamu Amaan Stadium Zanzibar na baadae jioni ni Taarab hapo hapo Uwanjani.
7-Ijumaa nyingine,Maharusi wakisindikizwa na ndugu,jamaa na marafiki kurejea Dar kwa Boti mbili za Kilimanjaro Seven na Eight na baadae wataelekea Msikiti mkuu wa Taifa Kinondoni kupata Swala ya Ijumaa na Dua toka kwa Mufti,,
Jioni yake Ramsa nyumbani kwa Bwana Harusi.
8-Jumamosi nyingine ndio kilele cha sherehe,Pale Benjamin Mkapa Stadium.
Mageti kufunguliwa Saa kumi na mbili alfajir,Wananchi kuanza kuingia Uwanjani,
Waalikwa na Viongozi kuja saa tatu na baadae ni Maulidi ya kinchi ikifuatiwa na lunch kwa Watu wote.
Jioni Saa moja ni Reception Kempinsk kwa Wageni na Watu mashuhuri tu.
Sioti ila kama Mwenyekiti wa kamati ya harusi nawaibia siri, Hv ndivyo itakavyokuwa Insha'Allah
@diamondplatnumz #OA
Comments