HUYU NDIYE WANU HAFIDH, CHAMPIONI WA ELIMU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, amemteua mbunge wa Makunduchi, Wanu Hafidh Ameir kuwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Swali; Wanu ni nani? Kwa nini yeye nafasi ya Naibu Waziri wa Elimu?

Jibu la kwanza ni hili; Wanu ni championi wa elimu.

Jibu la pili; Wanu ni shujaa wa nishati safi ya kupikia.

Wanu ni mwanasheria msomi. Kijamii ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF). Taasisi hiyo, imejikita katika kuwajenga na kuboresha maisha ya wanawake, vijana na watoto, kuanzia kwenye afya, elimu na uchumi.

Shabaha kubwa ya MIF ni kushughulikia matatizo ya kijamii ndani ya Zanzibar na Tanzania kwa jumla, kupitia utekelezaji wa mikakati ya kiulimwengu.

Madhumuni mama ya MIF ni kuzijengea uwezo jamii za Tanzania, kwa kuboresha elimu, kustawisha afya, kuchochea maendeleo ya kiuchumi, ili kuukabili na kuushinda umaskini, ujinga na maradhi, kupitia uongozi na juhudi za pamoja.

Jimbo la Makunduchi, Zanzibar, kabla hata Wanu hajawa mbunge, aliiongoza MIF, kuhakikisha inatokomeza matokeo ya sifuri kwa wanafunzi na shule za jimbo hilo. Alifanya hivyo kwa kuamini kwamba hiyo ni njia ya kimsingi ya kuboresha na kupandisha viwango vya elimu.

Wanu, anaamini kuwa tatizo kubwa ni ufaulu kwa watoto wa kike, na kwa sehemu kubwa chanzo chake ni umaskini, hivyo mpango wa muda mrefu wa MIF ni kuhakikisha mwanamke anapata ukombozi wa kimaisha.

Wanu alikuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar mwaka 2015 - 2020, akawa mbunge, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Baraza la Wawakilishi mwaka 2020 - 2025. Na Uchaguzi Mkuu 2025, Wanu aligombea ubunge jimbo la Makunduchi na kushinda.

Bila shaka, kwa jinsi ambavyo Wanu amekuwa akijitoa kwenye mapambano ya elimu, kupandisha hadhi ya elimu, kuchochea ufaulu wa wanafunzi, hasa wa watoto wa kike, imempendeza Rais Samia kumteua awe Naibu Waziri wa Elimu.

Hongera Wanu. Tunafahamu ulivyo mwanamapinduzi wa nishati safi ya kupikia, kuanzia shuleni hadi kwenye magereza ili kulinda afya za wafungwa. Hata hivyo, kujitoa kwako kwenye mapambano ya elimu, kumemfanya Rais Samia aone nuru ya Wizara ya Elimu, wewe ukiwa naibu waziri wake.

Nenda kapige kazi Championi Wanu.
Nenda ukaing’arishe elimu ya nchi, Championi Wanu.



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

WALIOCHUKUA FOMU CCM ZA KUWANIA USPIKA HAWA HAPA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MAWAZIRI WALIOACHWA HAWA HAPA

HISTORIA YA MAREHEMU MC PILIPILI

MJUE VIZURI KOCHA MPYA WA YANGA PEDRO

MATOKEO YA DARASA LA 7 YATANGAZWA