ZIJUE TABIA 9 ZA WANAWAKE HAWA....


Hii siri ikusaidie wewe na uzao wako

1. Mwanamke mwenye marafiki wa hovyo wanaopenda kuongea upupu tu. Angalia huko mtandaoni anahusiana na watu wa aina gani. Ukikuta mwanamke anaambatana na wanawake wa hovyo, yaani kwenye mambo ya hovyo kijingakijinga wanaitana na kumdhihaki mtu hamna mwanamke hapo huyo ni GARASA

2. MWANAMKE ambaye haishiwi changamoto kila leo zihusuzo pesa. Ukisema huna anakata simu au anakatisha maongezi na wewe kwa kujidai ana stress kisa ana uhitaji wa pesa. Hamnamo mtu hapo yaani kila leo amepata hili mara anadaiwa na mtu fulani msaidie alipe. Huyo ni mwanamke maslahi, akikosa pesa na uhusiano umekufa.

3. MWANAMKE asiyeweza kuheshimu utamaduni wenu, mwanamke anasema siwezi kuvaa gauni, kufunga kitenge, kupika ukweni kwenye kuni, siwezi kuchota maji nk. Ukiona familia aliyotokea kwanza inatia huruma ila anasema siwezi kupikia kuni, siwezi kuvaa gauni nimezoea vipesi au kuvaa suruali tu. Tupa kwenye shimo la takataka lala mbele usijifungamanishe naye, huyo sio mwanamke ni takataka katika maisha yako.

4. MWANAMKE anayetaka kujiamulia kisa anakuzidi kipato au madaraka yaani anataka kujiamulia ratiba zake au nini afanye kisa ana pesa na nini avae huku ni mke wako

5. MWANAMKE anayesema muoane na kila mtu akafanye ibada anakokujua eti ndoa haihusiani na ibada. Ukiona mwanamke ana kauli za kutengana kiimani achana naye, tafuta mtu sahihi ambaye anajua raha ya kuambatana na mume katika mambo yote.

6. MWANAMKE ambaye kila wakati anatoa kauli za kumbeza mwanaume, huyo achana naye. MATAMSHI au kauli za mwanamke zimebeba kiwango cha namna anavyokuheshimu na anavyokuchukulia kwenye maisha yake hayo.

Ukisikia au ukiona mwanamke anawadhihaki sana wanaume, anawahukumu sana wanaume katika ubaya, anaongea mwanaume kama hawezi kunifanyia hivi siwezi kuwa naye, mara wanaume wote ni mbwa tu nk 

7. MWANAMKE anayeamini kupewa kuliko kutoa, mbinafsi huyo ni mzigo sio TURUFU maana yeye ni msaidizi anakusaidia nini sasa. Mwanamke ambaye cha kwake chake na chako chenu. Mbinafsi mbaya mno hana THAMANI

8. MWANAMKE anayeongea kwa lugha za jeuri huyo si wako kwasababu hulka za mwanamke akiongea na mwanaume ampendaye kuna ulaini wa sauti na hekima humtawala sana anapozungumza na mtu anayemheshimu sana

9. MWANAMKE anayetanguliza kuomba pesa sana kila mnapotaka kuonana au mpokutana naye achana naye mnyonyaji huyo ni GARASA

Haya ni machache katika mengi, nyota njema huonekana asubuhi, mpime kwenye maongezi yake, aina ya marafiki zake wa mtandaoni na wale wa kawaida utajua huyo ni TURUFU au GARASA ili usije ukaingia choo cha kike mwanaume mwenzangu


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MWABUKUSI ATOA NENO SIMBA KUSUSIA DERBY DHIDI YA YANGA

RAIS TRUMP ARARUANA NA RAIS WA UKRAINE

SERIKALI YALIKUBALI OMBI LA DIAMOND

MWANAMKE ALIYEVUNJA REKODI KWA KUZAA WATOTO 69

HOSPITALI YA MUHIMBILI YAANZISHA HUDUMA YA KISASA YA KUZIBA MAPENGO

ARAJIGA AULA KOMBE LA DUNIA

BODI YA LIGI YAKIRI MAKOSA, WAIOMBA YANGA WAYAMALIZE