SAMATTA ALIA NA UWANJA WA AZAM UMEWAKOSESHA USHINDI


Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amesema kwamba udogo wa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam jana uliwakosesha ushindi dhidi ya Lesotho.
Taifa Stars usiku wa jana ililazimishwa sare ya 1-1 na Mamba wa Lesotho katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Uwanja wa Azam Complex.
Stars inayofundishwa na kocha Salum Mayanga, ilitangulia kwa bao la Samatta dakika ya 27 kwa shuti zuri la mpira wa adhabu, kabla ya Mamba kusawazisha kupitia kwa Thapelo Tale dakika  ya 34.
Nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta (kulia) amesema Uwanja uliwabana jana kucheza kwa uwezo wao 
Samatta baada ya mechi jana akiwa na mwandishi wa habari, Saada Akida

Na baada ya mchezo, Samatta akasema; “Uwanja wa azam Complex ni mdogo sana, kitu ambacho kwa upande wetu ambao wengi tumezoea kucheza Uwanja wa mkubwa wa Taifa  kimetufanya tujibane, tumeshindwa kucheza kwa uwezo wetu mechi ya leo, yaani ukipewa mpora ukigeuka, Uwanja umekwisha,”alisema.
Samatta pia akalaani staili ya ukabaji wa mabeki wa Lesotho, akisema walikuwa wanamfuata watatu kwa wakati mmoja hadi kuna wakati akajikuta anakasirika.
“Nimekasilrshwa na kitendo cha kutoka sare na Lesotho, sijafurahishwa kabisa ukiangalia tumecheza nyumbani na haikuwa akilini mwangu kama matokeo yangekuwa hivi, lakini ndio imekuwa hivi, tunawaahidi Watanzania tutafanya vizuri katika mechi zijazo,”alisema.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO

BREAKING: CAF YAIPOKONYA KENYA KUANDAA CHAN

BREAKING NEWSSSS. WABUNGE WAPATA AJALI

MONGELLA AWATEMBELEA HOSPITALI WALIOMWAGIWA TINDIKALI

π—₯π—”π—§π—œπ—•π—” 𝗬𝗔 π—¬π—”π—‘π—šπ—” 𝗬𝗔 π—žπ—¨π—™π—¨π—‘π—šπ—” 𝗠π—ͺπ—”π—žπ—” 2024 πŸ”°

GERSON MSIGWA AREJESHWA KUWA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI

AUCHO, BACCA, BOKA WAJUMUISHWA KWENDA ALGERIA LEO