ZIJUE FAIDA LUKUKI YA KILIMO CHA MCHAICHAI

SEMINA YA FURSA KILIMO NA UFUGAJI:
Mwalimu: Adam Ndamange
Products:
 • MCHAICHAI (LEMON GRASS)
• STRAWBERY
• MHOGO (CASSAVA)
• UFUGAJI WA WADUDU (INSECT)
• UYOGA
1. MCHAICHAI (LEMON GRASS):
Ni zao linalokubali kwenye ardhi ya kichanga na huchukua takribani miezi minne hadi kuvuna kwake.
Matumizi yake:
• Hutumika kama kwenye chai
• Hutumika kutengenezea sabuni
• Hutumika kutengenezea dawa za malaria
• Hutumika kutengenezea dawa za U.T.I
• Hutumika kutengenezea dawa za msongo wa mawazo
• Hutumika kutengenezea manukato (perfumes)
• Hutumika kutengenezea Airfresher kwa ajili ya matumizi ya salon, kwenye ndege, mabasi n.k
SOKO:
Kupitia Kampuni ya Kijani Kibichi kwa ushirikiano na Africafe, soko la zao hili linapatikana ndani na nje ya nchi. Kiwanda kipo Pemba-Zanzibar, Tanga na Kigamboni.
Kutokana na nia ya kutanua wigo wa zao hili, tayari Kampuni hii kwa ushirikiano na Africafe wako mbioni kujenga kiwanda maeneo ya Kibiti mkoa wa Pwani na tayari zipo kiasi cha Ekari 250 kwa ajili ya kulima Mchaichai.
Kwa kulima Ekari 1 ya zao hili ambayo huchukua miezi minne hadi kuvunwa kwake, matarajio yaliyopo ni kuvuna kiasi cha lita 10 za mafuta ya Mchaichai ambapo lita 1 inanunuliwa kwa kiasi cha TSH750,000.
MAUZO MAJANI MABICHI:
Aidha, Kampuni hiyo ya Kijani Kibichi inanunua kilo 1 ya mabaki ya majani mabichi ya Mchaichai kwa kiasi TSH500.
 Ekari 1 huweza kutoa 3,500kg hadi 4,000kg .
Makisio ya mapato ni kati ya 1,750,000 hadi 2,000,000
Majani mabichi huvunwa kila baada ya miezi mitatu ambapo kwa mwaka unaweza kuvuna mara nne.
MAUZO MAJANI MAKAVU:
Ekari 1 huweza kutoa kiasi cha 1,000Kg za majani makavu
Manunuzi kwa 1Kg ni kati ya TSH2,000 hadi TSH2,200
Mapato ni kati ya TSH2,000,000 hadi TSH2,200,000
MAJI YA MCHAICHAI:
• Hutengenezea Airfresher
• Hutengenezea Dawa za mbu
MANUNUZI YA MBEGU:
Kila kimti kwenye shina hununuliwa kwa kati ya =TSH20 hadi TSH30
GHARAMA ZA MCHAICHAI:
Kwanza ni lazima kuingia mkataba na Kampuni Kijani Kibichi ili kuweza kulima kibiashara
Ziko aina mbili za Mchaimchai;
• Mbegu ya Kitanzania; hii ni mbegu yenye sifa ya kutoa mafuta mengi ya Mchaichai lakini haina sifa ya kuhimili jua au ukame.
• Mbegu ya kutoka Afrika Kusini; hii ni mbegu ambayo inapatikana Zanzibar ambapo ina sifa ya kutoa mafuta kidogo lakini yenye kuhimili jua au ukame.
Tafti zinaendelea hivi sasa kupitia wataalamu wa Kampuni ya Kijani Kibichi ya kufanya CROSSBREEDING ya mbegu ya Mchaichai ya Tanzania na ile ya South Africa.
Aidha, kwenye mkataba kuna kipengele cha kupata mafunzo ya upandaji wa Mchaichai
Gharama za Mbegu:
• Mbegu ya Tanzania inapatikana kwa kiasi cha TSH450,000 kwa Ekari
• Mbegu ya South Africa inapatikana kwa kiasi cha TSH1,000,000 kwa Ekari
Mbegu hizi zitapatikana ndani ya siku 7 baada ya malipo na pia baada ya kupata vipimo vya udongo. Udongo unaofaa kwa kilimo cha Mchaichai ni udongo kichanga.
Ekari 1 inahitaji miche 6,000 huku idadi ya mashimo ikiwa ni 3,000.
GHARAMA NYINGINE:
Kugharimia Wataalamu kwa kuwalipa kiasi cha TSH120,000 kwa ajili ya;
• Kuna mafunzo ya awali ambapo kwa aliye tayari anatakiwa kulipa kiasi cha TSH80,000
• Kuna mafunzo ya vitendo (Practical Training),
• Kuna namna ya kufanya Pruning,
• Kumwagilia Mchaichai
• Kuna gharama za Uchimbaji wa mashimo chini ni futi 1 na Upana ni futi 2=TSH1,000 kwa shimo
GHARAMA YA MKATABA:
Mkataba unatakiwa kupelekwa kwa Mwanasheria kwa ajili ya kutiliana saini. Aidha mkataba huu ni flexible.
Gharama ya mkataba huu ni kiasi cha TSH250,000 kwa mwaka. Hata hivyo unatakiwa kulipa kwanza kiasi cha TSH75,000 na nyingine unatakiwa kulipa baada ya miezi mitatu TSH50,000 na kiwango kingine cha TSH50,000 baada ya miezi mitatu tena na hatimaye mwisho kabisa kumalizia kiasi cha TSH75,000.
Hivyo basi;
• Gharama za Mkataba za TSH250,000
• Gharama za Mbegu TSH450,000
• Gharama za Mafunzo TSH80,000
• Gharama za kujiunga Uanachama TSH10,000
• Gharama hizi ni za kati ya Ekari 1 hadi 5
APPROACH:
i). Kwa shamba la mmoja mmoja
ii). Kwa shamba la kikundi
Kutokana na fursa ya uwekezaji mkubwa wa Ekari 250 Kibiti kila mwanachama atalipa kiasi cha TSH395,000 kupitia Akaunti ya NMB ya Halmashauri ya Jiji kwa ajili ya ununuzi wa shamba na hatimaye kupata HATI. Hati ya umiliki wa shamba hutolewa baada ya miezi mitatu
Gharama za kusafisha shamba ni kiasi cha TSH720,000 kwa ekari
Mkataba wa kilimo cha Mchaichai ni wa miaka minne
GHARAMA YA MBEGU:
Gharma za kununua mbegu ni TSH75,000
Kiwanda kitawajibika kuvuna mafuta ya Mchaichai hapo hapo kwenye mashamba yaliyopo Kibiti
2. MIHOGO:
Kwa jina jingine zao hili la mhogo linaitwa WHITE GOLD.
1 Kg ya Mhogo hununuliwa lwa kiasi cha TSH1,150
Huchukua miezi 7 hadi 9 kuwa tayari kwa uvunaji
Kwa Ekari 1 huweza kutoa tani 10 hadi 12 na kununuliwa kwa TSH11 million
Mbegu inapatikana kupitia Kampuni ya Kijani Kibichi
Mbegu kwa Ekari ni TSh300,000
Gharama za Mkataba ni TSH150,000 na malipo yanaweza kufanywa kwa awamu tatu
Gharama ya mafunzo ni TSH50,000
Upandaji inatakiwa kuzingatia (vipingili vitatu kwenda chini na vitatu juu)
Lengo la Kampuni ni kuufanya mhogo kuwa zao kubwa la kibiashara
Aina nzuri za mbegu ni; KIROBA & MKURANGA II
3. STRAWBERY:
Ni zao kubwa la biashara
Linastawi katika mazingira ya baridi
1Kg hununuliwa kwa TSH20,000 hadi TSH25,000
Mche mmoja unagharimu kiasi cha kati ya TSH2,500 hadi TSH3,000.
Inatakiwa uwe na kiasi cha TSH600,000 kama gharama za mbegu kwenye Ekari 1
Zao hili huchukua takribani miezi mitatu hadi kukuwa kwake na kuuzwa
4. WADUDU
Hawa ni Mende na Funza ambao ni protein nzuri sana
Mende ana protein ya asilimia 85
Ni mbadala wa samaki na soya
Kampuni ya Kijani Kibichi iko kwenye mazungumzo na Interchick kwa ajili ya kusupply mende kama mbadala wa dagaa/samaki na soya kwa ajili ya kutengenezea chakula cha mifugo
Aina za Mende;
• Mende wa Kimarekani
• Mende wa Kijerumani
• Mende wa KiBongo (Kijani Kibichi)
Kwa maelezo zaidi google (Mende wa Kijani Kibichi)
Gharama;
Kupatiwa banda inagharimu TSH50,000
Mende 1 ni TSH1,000
Inatakiwa uwe na mende at least 20
Gharama ya mafunzo ni TSH80,000
Banda moja linachukua mende 100
1Kg ya mende ni TSH20,000
Chakula cha Mende hao ni Mabaki ya chakula
Mavuno ni kila baada ya miezi mitatu
Yai moja la Mende hutoa mende 300
Matumizi ya Mende;
• Hutengenezea dawa za mswaki
• Vipodozi
• Dawa za usingizi mahospitalini
• Pia hutumikak kwa tafiti maabara
5. UYOGA:
Aina za Uyoga;
• Mushroom
• Mama/Oyster
• Burtons
Ukila uyoga ni sawa umekula mboga 9
Kipindi kizuri kwa kupanda Uyoga ni kati ya March-August
Ni lazima uwe na Barcode unapouza uyoga sokoni
1Kg ya uyoga hununuliwa kwa TSH8,000
Uyoga huvunwa kila baada miezi mitatu
Uyoga unakuwa wenyewe
Ununuzi wa Mbegu ni kati ya TSH3,000 hadi TSH3,500
Minimum shamba linatakiwa liwe na chupa kati ya 50 ambapo chupa 1 hutoa mfuko mmoja wa uyoga
FAIDA:
Fresh Uyoga
Lotion ya Uyoga
Inatengenezea Unga wa Uyoga
Soko ni kutoka kwa Kampuni ya Kijani Kibichi
Gharama ya Mkataba ni TSH50,000
Gharama ya Mafunzo ni TSH30,000
Gharama ya manunuzi ya Mbegu ni TSH150,000
Gharama ya Banda ni kati ya TSH1,500,000 hadi TSH2,000,000
MAANDALIZI YA SEMINA NYINGINE
 Taarifa ya Maandalizi ya Semina nyingine kwa wakati mwingine itatolewa hivi karibuni
KIKUNDI CHA GREEN WINNERS
Semina iliazimia kuunda GREEN WINNERS GROUP, kikiwa na wajumbe 30.
LikeShow more reactions
Comment

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

JIONEE MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2015

CHANGAMKIA OFA YA KILIMO CHA PILIPILI KICHAA UPATE FAIDA SH. MIL. 50

NEWS ALERT: TAZAMA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2014 HAPA!

REKODI YA SIMBA NA YANGA TANGU MWAKA 2010

KAMBI YA MAFUNZO ELEKEZI KWA VIONGOZI 120 WA TGGA YAZINDULIWA KILIMANJARO+video