BENKI YA NMB YATOA MSAADA WA VITI NA MEZA 100 CHUO CHA AFYA MPANDA
Benki ya NMB imekabidhi msaada wa viti na meza 100 zenye thamani ya sh. Mil 10 kwa chuo cha afya Mpanda mkoani Katavi katika kusaidia uboreshaji wa miundombinu kwenye sekta ya Elimu na Afya kwa hapa nchini.
……………………………………………..
 
Makabidhiano hayo yalioongozwa na Meneja wa benki ya NMB kanda ya Magharibi, Sospeter Magese na kushuhudiwa na mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko yalifanyika chuoni hapo Mwishoni mwa wiki iliyopita.
 
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Bw. Sospeter alisema kuwa imekuwa desturi ya benki ya NMB kutenga asilimia moja ya faida yake baada ya kodi kwa ajili ya kusaidia jamii inayowazunguka kwani jamii hizo ndio zimeifanya benki ya NMB kuwa benki kinara hapa nchini.
 
“kwa zaidi ya miaka saba sasa tumekuwa tukitenga asilimia moja ya faida ya benki kwaajili ya kusaidia jamii zetu katika nyanja za elimu, afya na kunapotokea majanga mbalimbali. Kuzisaidia jamii zetu imekuwa desturi yetu kwani jamii hizi ndizo zimekuwa chachu kubwa ya sisi kama benki ya NMB kufanya vyema na kufika hapa tulipo,” alisema.
 
Mbali na misaada kwa jamii, Meneja huyo alisisitiza juu ya mikopo rafiki inayotolewa na benki ya NMB katika sekta ya kilimo na ufugaji huku akasisitiza juu ya kuchukua mikopo hii kwani ndio chachu ya maendeleo ya uchumi.
 
Aidha, Mkuu wa mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko aliipongeza benki ya NMB kwa moyo wao wakujitoa na kusaidia jamii zao huku akiwashukuru kwa msaada walioutoa kwa chuo cha afya Mpanda na kuisihi benki ya NMB kutochoka kusaidia jamii na hususani mkoa wa Katavi.
 
Bi Mrindoko alisema, “Binafsi niwapongeze sana kwa kujitoa kwenu kwani mmekuwa ni chachu ya maendeleo kwa mkoa wetu, tunazidi kuwashukuru sana na kuwaomba msichoke kuzisaidia jamii za Kitanzania na ikiwapendeza mzidi kuleta misaada katika sekta hizi za Afya na elimu kwa mkoa wetu wa Katavi.”
 
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho, Lightness Michael aliiomba benki ya NMB kuendelea kutoa misaada kwa chuo hicho kwani bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo uchache wa madarsa ambao kama utatatuliwa basi wataongeza udahili wa wanafunzi katika chuo hicho.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

HIZI NDIO DALILI ZA VVU KWA WATOTO WADOGO

MAMBO YA BUNGENI DODOMA LEO+video

REKODI YA SIMBA NA YANGA TANGU MWAKA 2010

PROF. NDAKIDEMI: TUKIACHA KABISA KINGEREZA KUFUNDISHIA, TUTAPIGWA GOLI KIMATAIFA+video

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013 YATOKA, YAPO HAPA ... YAONE HAPA KWA NJIA RAHISI KABISA

WAZIRI MKUU MGENI RASMI KONGAMANO LA KUMBUKIZI YA BABA WA TAIFA HAYATI JULIUS NYERERE+video

DKT MPANGO AIPONGEZA WIZARA YA ELIMU, AWAKABIDHI MAMILIONI WABUNIFU

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

MAGESSA: TUNAOMBA SERIKALI ITUPATIE MAAFISA UGANI, SKIMU ZA UMWAGILIAJI BUSANDA+video