BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi akilakiwa kwa furaha na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho ambaye hivi sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo wakati wa mapokezi kwenye mkutano wa hadhara mjini Tunduma wakati wa ziara ya kikazi mkoani Songwe Aprili 15, 2024.

Dkt. Nchimbi ambaye ameambatana na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla pamoja na Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu ameanza ziara ya kikazi ya siku kumi katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.

Lengo la ziara hiyo ni kuhuisha uhai wa chama, kutatua kero za wananchi, kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.

Baada ya kumaliza katika mikoa ya Katavi, Rukwa na Songwe, ziara hiyo ya siku 10 yenye mafanikio makubwa, itaendelea kesho katika Mkoa Mbeya na hatimaye katika mikoa ya Njombe na Ruvuma.
Chongolo akiwatambulisha viongozi wa mkoa huo
Dkt Nchimbi akizungumza jambo na Chongolo
Chongolo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kwa Mkoa huo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Nchimbi wakati wa mkutano wa hadhara mjini Tunduma.



Chongolo akisikiliza kwa makini wakati Dkt Nchimbi akihutubia
Chongolo akizungumza na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla.


Katibu wa Oganaizesheni akisalimiana na Chongolo
Dkt Nchimbi akiwa na Chongolo walipokuwa wakiondoka baada ya mkutano kumalizika

 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA

0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI