MANJI: SIWEZI KURUDI TENA YANGA SC


 

Mwenyekiti na Mfadhili wa zamani wa Young Africans, Yusuf Manji amesema kwa sasa hafikirii kurejea ndani ya klabu hiyo ingawa anafurahia kuona imekuwa na umoja na mshikamano wa hali ya juu.


Manji amesema kwa sasa umri wake unambana kujiweka karibu na timu hiyo na soka kwa ujumla, hivyo anaendelea kujishughulisha na mambo mengine.


"Kwa sasa siwezi, kwanza umri umeenda siwezi zile pilikapilika za kusimamia timu," amesema Manji aliyeiongoza Young Africans kwa miaka minne.


"Unajua hata kama utakuwa ofisini, tabia yangu ni kwamba napenda kufanya kazi zote nikiwa karibu. Naweza kuwa na viongozi wengine lakini nitalazimika kusafiri na wachezaji, nahakikisha kila kitu chao kinaenda vizuri, ukweli kwa kipindi hiki sitakuwa na uwezo tena wa kufanya hivyo wanatakiwa kufanya vijana."


Manji amesema kuwa pamoja na hilo, anafurahia kuona klabu hiyo ina umoja wa hali ya juu kwa sasa jambo ambalo lilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu.


"Moja ya jambo ambalo nakumbuka nililifanya na kuisaidia Young Africans hii kufika hapa ni kuweka umoja, wakati naingia nilikuta migogoro mingi kuliku makundi matatu, nakumbuka moja liliitwa Yanga Asili, lingine Kampuni moja liliitwa Yanga Akademia.


“Nilitumia ushawishi na wangu wote na kuhakikisha haya makundi yanaisha na Young Africans ikasimama, nafikiri imewasaidia hadi leo ndiyo maana kuna umoja," amesema Manji.


Credit, #Dar24.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA