DKT NCHIMBI KUWEKA MSUKUMO UJENZI KITUO CHA AFYA MBAHA, NYASA



Shamra shamra za kumkaribisha Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi alipowasili kwao katika Kata ya Mbaha, wilayani Nyasa Ruvuma alipokwenda kuwasalimia wananchi wakati wa ziara ya kikazi Aprili 21, 2024.

Baada ya kusikiliza kero za wananchi wa eneo hilo aliwashukuru kwa mapokezi mazuri yaliyoambatana na ngoma mbalimbali za asili, alisikiliza kero za wananchi na baadhi kuzitafutia ufumbuzi kwa kuwaita viongozi wa Taasisi kujibu majibu sahihi na jinsi ya kuzitatua.

  Kero zilizowasilishwa  ni  uhaba wa maji, miundombinu ya barabara na ujenzi wa Kituo cha Afya eneo hilo ambacho aliahidi kuweka msukumo wa kipekee kuhakikisha kinajengwa haraka kunusuru vifo vya wagonjwa wanaosafirishwa umbali mrefu kwenda kupata matibabu katika vituo ama hospitali za mbali..

Katika ziara hiyo, Dk Nchimbi ameambatana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu na Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha, Dk Frank Hawasi.

Lengo la ziara hiyo ya siku 10 katika mikoa 6 ni kuimarisha uhai wa chama kuanzia ngazi ya mashina, kusikiliza kero na kuzitafutia ufumbuzi, kuelezea maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani, kukagua miradi ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM


Dk Nchimbi akiangalia na kufurahishwa na ngoma mbalimbali za asili ikiwemo mganda, chihoda







Akitia saini katika kitabu cha kumbukumbu
Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Stelah Manyanya akielezea mambo mengi ya maendeleo yaliyonywa wakati wa kipindi chake cha uongozi katika jimbo hilo.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Dk Nchimbi kuanza kuzungumza na wananchi.


Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu akielezea umuhimu wa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura.



Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha, Dk Frank Hawasi.


 Dk Nchimbi akizungumza na wananchi wakati wa mapokezi yake


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA

0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA

DKT NCHIMBI AZURU KABURI LA JOHN KOMBA LITUHI, NYASA

DKT NCHIMBI AAGIZA UJENZI UWANJA WA NDEGE SUMBAWANGA UKAMILIKE HARAKA