KIJIJI CHA KATARYO CHAONGEZA KASI YA UJENZI WA ZAHANATI YAKE: MBUNGE AKICHANGIA SARUJI MIFUKO 200





 

Kijiji cha Kataryo ni moja ya vijiji vitatu vya Kata ya Tegeruka. Vijiji vingine ni: Mayani na Tegeruka.


Kijiji cha Kataryo hakina zahanati yake, kwa hiyo wakazi wake wanalazimika kusafiri umbali wa zaidi ya kilomita saba (7) kwenda kupata Huduma za Afya kwenye zahanati ya kijiji jirani cha Mayani.


*Kijiji cha Kataryo chaamua kujenga Zahanati yake:*

Ujenzi ulianza rasmi Julai 2023, na Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo alikaribishwa kupiga Harambee ya kuchangia ujenzi huo tarehe 4.4.2024


Wakazi wa Vitongoji sita (6) vya Kijiji cha Kataryo walikubaliana kuchangia vifaa vya ujenzi kulingana na wingi wa kaya za kila kitongoji. Michango ya awali ilikuwa kati ya Shilingi 5,000 na 7,000 kwa kila kaya.


*Matokeo ya Harambee ya Mbunge wa Jimbo:*

Harambee ilifanyika tarehe 4.4.2024 na matokeo yake ni:


(i) Saruji kutoka kwa Mbunge wa Jimbo:

     Saruji Mifuko 200

(ii) Saruji kutoka kwa Diwani, Mhe Alpha Mashauri

       Saruji Mifuko 50

(iii) Saruji kutoka kwa wanakijiji:

       Saruji Mifuko 26

(iv) Fedha: Shilingi 600,000 


*Akaunti ya kuwasilisha michango yetu ya fedha:*

Wana-Kataryo na Wadau wengine wa Maendeleo wanaombwa kutoa michango  yao kupitia Akaunti ya Kijiji ambayo ni:


Benki: NMB

Akaunti Na: 30302300302

Jina: Kijiji cha Kataryo


*Huduma za Afya Jimboni mwetu:*

Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 zenye Vijiji 68 lina:


*Hospitali 1 ya Halmashauri yenye hadhi ya hospitali ya Wilaya


*Vituo vya Afya: 6


*Zahanati za Serikali: 25

*Zahanati Binafsi: 4


*Zahanati zinazojengwa: 16


*Picha za hapa zinaonesha:*

*Boma la OPD la Zahanati inayojengwa Kijijini Kataryo, Kata ya Tegeruka 


*Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini akitoa majibu ya kero na matatizo ya wananchi kabla ya kuanza kupiga Harambee ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kataryo 


*Wananchi wa Kata ya Tegeruka wakiwa wamegawiwa vitabu viwili viwili (Volumes III & IV) vinavyoelezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025 ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.


Ofisi ya Mbunge 

Jimbo la Musoma Vijijini 

www.musomavijijini.or.tz 


P. O. Box 6

Musoma 


Tarehe:

Jumapili, 28.4.2024

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

YANGA BADO POINTI 2 TU ITANGAZE UBINGWA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA

DKT NCHIMBI AZURU KABURI LA JOHN KOMBA LITUHI, NYASA

MWANACHADEMA MSEMAJI WA WAMACHINGA TAIFA AHAMIA CCM