KILICHOSABABISHA YANGA KUTOSHIRIKI KOMBE LA MUUNGANO...


 

Klabu ya Yanga SC haitashiriki michuano ya Kombe la Muungano mwaka huu kwa sababu ya ratiba klabu hiyo kuwabana sana tofauti na klabu nyingine kubwa za Simba SC na klabu ya Azam FC. Klabu ya Yanga SC ina Kombe la Shirikisho (FA Cup) na Ligi Kuu, wakati huo klabu ya Azam FC ina FA Cup na Ligi Kuu lakini tayari yupo mbele kwa michezo miwili (2) ya Ligi Kuu, huku klabu ya Simba SC ikiwa imesalia na Ligi Kuu pekee na haina FA Cup bila kusahau uwezekano wake wa kushinda ubingwa msimu huu kuwa mdogo mno.


Klabu ya Simba SC ina michezo (21) ya Ligi Kuu haina FA Cup, klabu ya Yanga SC ina michezo (22) ya Ligi Kuu na FA Cup, klabu ya Azam FC ina michezo (24) ya Ligi Kuu na ina FA Cup. Kwa maana hiyo changamoto ni ratiba kuwa ngumu mno kwa klabu ya Wananchi ndio maana hawatoshiriki mwaka huu na sio vinginevyo.


- klabu zitazoshiriki kombe la Muungano msimu huu ni :


1. Simba SC (Tanzania Bara)

2. Azam FC (Tanzania Bara)

3. KVZ FC (Zanzibar)

4. KMKM (Zanzibar)


- Ratiba ya michuano hiyo 


* KVZ FC Vs Simba SC (24/4/2024, Saa 2:15 Usiku)

* Azam FC Vs KMKM (25/4/2024, Saa 2:15 Usiku)


* Fainali Itachezwa tarehe 27/4/2024 majira ya Saa 2:15 Usiku kwenye Uwanja wa New Amaan Complex Visiwani Zanzibar (Pamoja na michezo yote).



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA