UHUSIANO KATI YA TANZANIA NA NCHI MBALIMBALI UMEENDELEA KUIMARIKA NDANI YA MIAKA 60 YA MUUNGANO

NAIBU WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Nassor Mbarouk akizungumza na wanahabari leo April 18,2024 jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Picha na Manase Madelemu)

NAIBU WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor amesema kuwa tunapoadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanzania bara na Zanzibar uhusiano Kati ya Tanzania na nchi mbalimbali umeendelea kuimarika.

Balozi Mbarouk Nassor amesema hayo leo April 18,2024 jijini Dodoma wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu mafanikio ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Amesema kuwa Tanzania imeendelea kufungua Balozi na Ofisi za Uwakilishi katika nchi mbalimbali za kimkakati ikiwa ni sehemu ya kuimarisha utekelezaji wa Sera ya mambo ya nje hususani diplomasia ya Uchumi.

"Serikali ya awamu ya sita imefungua Balozi Mpya mbili za Vienna, Austria na Jakata, Indonesia na Konseli kuu mbili za Lugumbashi na Guangzhou China,ufunguzi wa Balozi hizo umeifanya Tanzania kufikisha jumla ya Balozi na Ofisi za Uwakilishi zipatazo 45 na Konseli kuu tano"amesema

Kadhalika amesema kuwa Tanzania ni mwenyeji wa nchi na Mashirika ya Kimataifa zaidi ya 90 ikiwemo Konseli kuu ambazo baadhi yake zipo Zanzibar kama vile China,Oman, Indonesia na Umoja wa Falme za kiarabu.

"Uwepo wa Konseli kuu amechangia kuimarika kwa manufaa katika sekta za Ushirikiano ikiwemo biashara, Utalii, uwekezaji, uchumi wa buluu na kubidhahisha Kiswahili"amesema

Kuhusu kubidhahisha Kiswahili duniani amesema kuwa katika kipindi cha miaka 60 ya Muungano Tanzania imechangia katika juhudi za kubidhahisha Kiswahili ndani na nje ya nchi ikiwemo kutoa ushawishi wa matumizi ya lugha hii kama nyenzo ya diplomasia,usuluhishi wa migogoro ukombozi na Uhuru katika nchi katika nchi za bara la Afrika.

Vile vile Kiswahili kuwa lugha rasmi katika Umoja wa bara la Afrika, Jumuiya ya Afika Mashariki, Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika.

"Tanzania imefanikiwa kushawishi dunia kupitia UNESCO ambapo imeitambua tarehe 7 Julai kila mwaka kama siku ya Kiswahili duniani"amesema

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Balozi Nassor Mbarouk ametoa rai kwa wanahabari na wananchi kwa ujumla kuendelea na moyo wa Uzalendo kuitangaza Tanzania Kimataifa na kuendelea kuuenzi Muungano ambao ni wa kipekee duniani.

(Imeandikwa na Manase Madelemu)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI