WANANCHI WA KAWAIDA KUFAIDI TRENI YA UMEME KWA NAULI NAFUU


Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amewaeleza wabunge kuwa serikali itahakikisha nauli ya Treni ya Umeme inakuwa ya chini hasa kwa wananchi wa kawaida ili nao wafaidi kasi ya mwendo wa  Km 160 kwa saa.


Ametoa uhakika huo alipokuwa akijibu maswali wakati wa semina kwa wabunge iliyoandaliwa maalumu kuelezea maendeleo ya ujenzi mradi huo mkubwa wa SGR iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Msekwa bungeni Dodoma Mei 4, 2024.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa akifafanua jambo alipokuwa akijibu maswali ya wabunge wakati wa semina hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Seleman Kakoso akihitimisha semina hiyo kwa kutoa maelekezo kwa serikali kuyafanyia kazi baadhi ya mambo ili ujenzi ukamilike.
Baadhi ya wabunge waliohudhuria semina hiyo wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha ujenzi wa mradi huo wa SGR unakamilika kwa mafanikio.






 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA-0754264203

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
 MSIMAMIZI MKUU 
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
 0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

YANGA BADO POINTI 2 TU ITANGAZE UBINGWA

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA

DKT NCHIMBI AZURU KABURI LA JOHN KOMBA LITUHI, NYASA

ZIARA YA DKT NCHIMBI KUINGIA RUVUMA LEO