ZIARA YA DKT NCHIMBI KUINGIA RUVUMA LEO


 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapimduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye leo anamalizia ziara yake mkoani Njombe, baadaye mchana anaingia mkoani Ruvuma kwa kufanya mkutano wake wa hadhara katika Jimbo la Madaba.

Kabla ya kuondoka Njombe atafanya kikao na Kamati ya Siasa itakayotoa Taarifa ya chama na serikali ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Mkoa huo ya miaka mitatu na kufuatiwa na mkutano ndani.

Katika ziara hiyo, Dkt. Nchimbi  ameambatana na wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla pamoja na Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu.

 Kiongozi huyo mtendaji mkuu wa CCM, atakuwa mkoani Ruvuma ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya siku 10 katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.

Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha uhai wa chama, kutatua kero za wananchi, kuelezea maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani, kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.

Baada ya kumaliza katika mikoa ya Katavi, Rukwa na Songwe na Mbeya, ziara hiyo ya siku 10 yenye mafanikio makubwa, itaendelea leo asubuhi katika Mkoa wa Njombe na hatimaye mchana kuingia katika Mkoa wa Ruvuma.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE