PROF MUHONGO AMEJIANDIKISHA KUPIGA KURA TAREHE 27.11.2024*





 *

Leo, Ijumaa, 11.10.2024, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, amejiandikisha kupiga kura tarehe 27.11.2024.

Vilevile, ametembelea vitongoji kadhaa vya Kata nne, ikiwemo Kata ya kwao ya Kiriba, yenye vijiji 3 na vitongoji 24, na kupata yafuatayo:

(i) Idadi ya wapiga kura waliojiandikisha ndani ya Kata ya Kiriba kwa siku ya leo:  1,856

(ii) Idadi ya wapiga kura waliojiandikisha kwenye Kitongoji cha Miembeni (Kituo cha Afya), Kijiji cha Bwai Kwitururu
     Kufikia saa 6 mchana: 22
     Kufikia saa 12 jioni: 50
Prof Sospeter Muhongo amejiandikisha hapo

*Uhamasishaji:*
Wananchi waendelee kuhamasishwa kujitokeza kujiandikisha kupiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa tarehe 27.11.2024

*Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:*

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, akijiandikisha kupiga kura, na kutembelea vituo kadhaa vya uandikishaji wapiga kura ndani ya kata nne za Musoma Vijijini.

Ofisi ya Mbunge 
Jimbo la Musoma Vijijini 
www.musomavijijini.or.tz 

P. O. Box 6
Musoma 

Tarehe:
Ijumaa, 11.10.2024

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

KIKOSI CHA CBE KIMEWASILI ZENJI KUVAANA NA YANGA

NDOGO WA MUME WANGU ALIKUWA EX WANGU

TAKUKURU YAPONGEZWA KUWA BEGA KWA BEGA NA MBIO ZA SEPESHA ZINAZOPINGA RUSHWA YA NGONO