KAMPENI YA UJENZI WA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI KWENYE SEKONDARI ZA KATA MUSOMA VIJIJINI




Ukubwa wa Jimbo la Musoma Vijijini
Kata 21 zenye vijiji 68 na vitongoji 374

Idadi ya Shule za Sekondari
Sekondari za Kata/Serikali: 26
Sekondari za Binafsi: 2
Sekondari mpya zinazojengwa: 12

Idadi ya Maabara za Masomo ya Sayansi (physics, chemistry & biology) kwenye Sekondari za Kata

Maabara zinazohitajika: 78
Maabara zilizopo: 41

(i) Sekondari 7: zina maabara tatu
(ii) Sekondari 8: zina maabara mbili
(iii) Sekondari 4: zina maabara moja
(iv) Sekondari 7: hazina maabara

Kampeni ya ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi

Wananchi na viongozi wao wanashirikiana na Serikali kuharakisha ujenzi wa maabara tatu kwenye kila Sekondari ya Kata. 

Ujenzi unaendelea na Mbunge wa Jimbo anaendelea kupiga Harambee za ujenzi huu.

(i) Sekondari ambazo hazina maabara ni:
Bukwaya, Busambara, Mtiro, Murangi, Nyanja, Seka na Tegeruka 

(ii) Sekondari zenye maabara moja ni:
Bukima, Dan Mapigano, Kasoma na Mabuimerafuru 

WITO WA KUCHANGIA
Wadau wa Maendeleo na hasa Wazaliwa wa Musoma Vijijini wanaombwa wajitokeze kuchangia ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi kwenye Sekondari zetu za Kata.

Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:

Baadhi ya maabara zilizojengwa kwa ushirikiano mzuri wa wanavijiji, viongozi wao na Serikali yetu.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini 
www.musomavijijini.or.tz 

Tarehe:
Jumapili, 6.10.2024




 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

𝗠𝗕𝗢𝗪𝗘 𝗔𝗦𝗜𝗧𝗜𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗔𝗡𝗗𝗔𝗠𝗔𝗡𝗢 𝗬𝗔 𝗖𝗛𝗔𝗗𝗘𝗠𝗔 𝗬𝗔 𝗧𝗔𝗥𝗘𝗛𝗘 𝟮𝟯.

KAMATI YA UWT KUTOA MSAADA WA KISHERIA NCHINI

KIKOSI CHA CBE KIMEWASILI ZENJI KUVAANA NA YANGA

YANGA YAWASILI SALAMA ETHIOPIA

MAYELE AIMWAGIA SIFA LUKUKI YANGA